ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 19, 2014

Kila kijiji ndani ya Jimbo la Chalinze kupata Trekta kwa ajili ya Kilimo – Ridhiwani Kikwete


TALAWANDA 1 (5)
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete (kushoto) akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Mindukene,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze leo Machi 18,2014.Katika Mikutano yake kwenye Vijiji vya Mindukene, Msigi na Kisanga ndani ya Jimbo hilo,Ridhiwani Kikwete ameahidi kuhakikisha vijiji vyote kwenye jimbo hilo vinakuwa na matrekta ili kuboresha kilimo.(Picha na Othman Michuzi).
MGOMBEA wa Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwenye Jimbo la Chalinze wilayani Bagamoyo mkoani Pwani, Ridhiwani Kikwete ameahidi kuhakikisha vijiji vyote kwenye jimbo hilo vinakuwa na matrekta ili kuboresha kilimo kiwe na tija.
Alitoa ahadi hiyo wakati wa mikutano ya kampeni kwenye vijiji vya Mindukene, Msigi, Kisanga vyote vikiwa kwenye  kata ya
Talawanda.
Kikwete alisema kuwa wakulima wengi bado wanatumia jembe la mkono ambalo haliwezi kuwaletea manufaa wala kuboresha kilimo ambacho ni tegemeo lao.
“Nikianikiwa kupata ubunge nitahakikisha kila kijiji kinakuwa na matrekta kwa ajili ya kuwa na wakulima ambao wataweza kulima kwa faida kwa ajili ya chakula na ziada kuuza ili kujiongezea kipato,” alisema Kikwete.
TALAWANDA 1 (6)
Akizungumzia changamoto ya migogoro ya wakulima na wafugaji alisema kuwa atahakikisha anazikutanisha pande zote ili kujua chanzo cha migogoro hiyo.
“Tatizo kubwa ni viongozi kushindwa kuzikutanisha pande zinazohusika badala yake wanaongea na upande mmoja jambo ambalo haliwezi kumaliza migogoro hiyo ambapo njia pekee ni kuwa na matumizi bora ya ardhi kwa kutenga maeneo kwa wakulima na wafugaji,” alisema Kikwete.
Aidha alisema kuwa migogoro hiyo inatokana na wafugaji kuingia kinyemela pasipo kufuata taratibu bila ya kupitia kwenye mikutano mikuu ya serikali za vijiji.
TALAWANDA 1 (8)
Mgombea Ubunge wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mzee Joseph January wa Kijiji cha Kisanda,Kata ya Talawanda ndani ya Jimbo la Chalinze.(Picha na Othman Michuzi).
Katika hatua nyingine aliwataka wazazi kuepukana na tabia ya kuuza kiholela maeneo yao hali ambayo itasababisha vijana kukosa ardhi kwa ajili ya kilimo na makazi.
Aliongeza kuwa atahakikisha anaboresha masuala mbalimbali ikiwemo sekta ya elimu, afya, miundombinu, kilimo, mikopo kwa  vijana na akinamama, uzinduzi rasmi wa kampeni unatarajiwa kufanyika kesho Aprili huko Chalinze na uchaguzi utafanyika Aprili 6 mwaka huu.

5 comments:

Anonymous said...

Corruption, hayo matreka yatatoka wapi kwa pesa za nani?

Utamu said...

Baba yake pamoja na kuwa mbunge na rais kashindwa ndio yeye?
Hizi hadithi za wanasiasa za "kuondoa umasikini" zinawapumbaza sana watz mabwege
Anataka ubunge aweze kupiga dili kiulaini basi!

Anonymous said...

Wananunua kura. Iwe illigal kuwapa watu vitu wakati wa campaign. This is wrong

Anonymous said...

Rushwa inaruhusiwa kwenye kampeni za uchaguzi!!!??

Anonymous said...

mtasema sana na kuandika kila maneno ya kweli lakini mwisho wa siku ndo hao hao watakao kuja kutawala angalia wanaotawala na walioa tawala zamani ni wakina nani?
ndo maana mpaka hii leo namuheshimu sana mwalimu nyerere jinsi alivyowalea vema watoto wake huwaona kupayuka payuka ovyoo kama mbwa mwitu wanasaka mfuka.mungu mbariki sana huko alipo na mlaze mahali pema peponi mwalimu nyerere baba yetu wa taifa for ever alikuwa kweli ana mapungufu yake lakini si kama hawa watoto wa mafisadi