Madereva Bajaj wakiwa nje ya ofisi za chadema makao makuu kinondoni wakipinga tamko la kuzuiwa kuingia kati kati ya mji na maeneo ya mjini.
Polisi wakiwa wamefika eneo la tukio mda huu ili kuweza kuweka hali ya usalama na kuzuia vurugu
Waendesha bodaboda na bajaj jijini dar mda huu wameandamana mpaka Ofisi za chadema makao makuu kinondoni,Nia ya maandamano yao hayo ni kupinga tamko linalowataka kutopeleka abiria maeneo yote ya kati kati ya jiji la dar.Mmoja wa madereva hao akiongea na mtandao wetu anasema kwamba wameamua kuandamana mpaka ofisi za chadema kwa kuwa wanaamini ndio watapata msaada.Taarifa kamili na picha zaidi zitakujia inakujia hivi punde.HABARI NA DJ SEK BLOG



5 comments:
Hoja ya serikali kukataza bodax2 kuingia city centre niya msingi na mimi binafsi naiunga mkono.Na ujinga wa hawa madereva kutaka kuigeuza hoja hii kuwa ya kisiasa ndipo wanapoonyesha umbumbu wao.
Tumechoshwa na misongamano ya bodaboda na bajaji mijini vilex2 wara kadhaa wamekuwa wakitumiwa na majambazi kuwapora watu vijisenti vyao mara wanapotoka kwenye mabenki.
mimi naunga mkono hoja boda boda wasiingie mji hayo ndio maandeleo,-
Mara hii serikali inafanya kazi
hoja hii ni ya msingi sana kwani hii ni kwa ajili ya usalama wetu sisi wenyewe, ndugu watanzania wenzangu tuache ubishi kwani matukio ya uharifu yanayofanika katikati ya mji kwa kutumia hizihizi bodaboda hatuyaoni?
Post a Comment