Ø ATAO WITO KILA MKOA UJITAMBULISHE KWA
ZAO LAKE,
Ø AWANANGA CHADEMA KUWA WAASISI WA
SIASA ZA UKANJANJA.
Ø AMPONGEZA TUNDU LISU KWA KUWA KIONGOZI MJANJA.
Ø AKABIDHI KADI 50 KWA
VIJANAWALIOJIUNGA NA CHAMA CHA MA PINDUZI (CCM) NA KUVUNA WANACHAMA WENGINE KUTOKA
CHADEMA.
Katibu
wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi wa jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama
Cha Mapinduzi (UVCCM) ambae pia ni Mjumbe wa Bunge Maalum la katiba Ndugu Paul
Makonda amefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Singida na kusimika makamanda
wateule wa jumuiya ya Vijana wa Kata 16 za wilaya ya Singida Mjini.
Shughuli
hiyo ya kusimika makamanda 16 iliyofanyika Katika Mkutano wa hadhara katika
uwanja wa Ukombozi uliopo Kata ya Majengo Singida Mjini ilihudhuriwa na mamia ya wananchi ambao
walijitokeza kumsikiliza kiongozi huyo wa Jumuiya ya Vijana.
Akiongea
na wananchi, Paul Makonda amewataka Makamanda hao wateule kufanya kazi kwa
ajili ya Jumuiya, Chama na wananchi, amewataka watambue kuwa nafasi hiyo ni kubwa
na ya msingi kwa Maendeleo ya Vijana na wananchi kwa Ujumla.
Lakini
pia amewataka wananchi wa Singida na watanzania wa mikoa yote kujitambulisha
kimikoa katika sura ya kimataifa kwa aina ya zao wanalozalisha, aliwataka wanasingida
kujitambulisha kwa zao la alizet na kutumia kilimo kama nyenzo muhimu ya
kijiletea Maendeleo ya Kiuchumi.
Katika mkutano huo, Makonda alikabidhi kadi kwa
vijana Zaidi ya 50 ambao waliamua kujiunga na Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa
Chama Cha Mapinduzi na kupokea wanachama wengine kutoka Chama Cha Demokrasia na
Maendeleo (CHADEMA) wakiongozwa na kiongozi wa Vijana wa CHADEMA wa Kata hiyo
ndugu Yasin Athuman.
Pia,
aliwananga Viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kuacha za
Ukanjanja za kutumia matatizo ya wananchi kama daraja la kufikia mafanikio yao
binafsi. Asema wanashindwa kutumia rasilimali zao kujiimarisha kama Chama na
kusaidia kutatua matatizo ya wananchi badala ya kutumia fedha nyingi kwa kukodi
helkopta na kufanya matumizi yasiyo na msingi yasiyojali mustakabal mwema wa
Wananchi. Pia amsifu na kumpongeza Tundu
Lissu kuwa ni kiongozi mjanja ndani ya Chama hicho kwani baada ya kugundua kuwa
Chama hicho kinaendeshwa kiukoo na kifamilia nae akamchukua Dada yake anayeitwa
Christina Lissu na kumpa Ubunge wa Viti maalum.
No comments:
Post a Comment