ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, March 25, 2014

Michael Agustine Lukindo Mtanzania aliyefariki Wisconsin wanatafutwa ndugu zake maiti kuchomwa moto Jumamosi

Michael Agustine Lukindo enzi ya uhai wake.
Kuna Mtanzania mwenzetu amefariki Madison Wisconsin nchini Marekani, wanatafutwa ndugu zake. ni mtu wa Tanga Michael Agustine Lukindo. Alikuja USA miaka mingi iliyopita, inasemekana zaidi ya miaka thelathini. Ameacha mke (African American) na watoto wanne, mkubwa alizaliwa 1989 familia yake haijui ndugu za Michael. Mazishi yatafanyika Jumamosi March 29, 2014, ila mwili utachomwa. Kama unafununu au kujua lolote kuhusiana na ndugu yetu huyu unijulishe mimi naitwa Lugome Fautus email yangu ni g5state@yahoo.co.uk . Lengo nikuweza kuwafahamisha ndugu zake nyumbani Tanzania na popote pale walipo. Asante kwa ushirikiano wako. Tunatanguliza shukurani
Michael Lukindo akiwa na mkewe na watoto wake wanne.
Historia yake
Augustino “Mike” Lukindo, 59 , departed this life on Sunday, March 16, 2014, surrounded by his immediate family. Mike was born and raised in Tanzania, Africa (Tanga) to Augustino and Josephine Lukindo. He moved to America in the early 1980’s, where he lived in Providence, Rhode Island for five years. Mike married Lillie B. in Rhode Island, and later moved to Madison where they built their family of four and confessed his life to Christ.
Mike was a family man, a funny guy with a good sense of humor. He loved to joke around. He liked comedy and he loved going to his children’s school to participate. He always had a smile and his favorite phrases were “Hey Brother-in-law , Sister-in-law, where the party at?” Mike was of true African decent, he never forgot his heritage.

Augustino “Mike” was proceeded in death by his mother, father, siblings and one sister-in-law, Irlene Person-Wilson. Mike is survived by his wife Lillie, son Augustino Franklin, three daughters Amanda, Josephine and Adrian Lukindo, all of Madison.

Kwa taarifa zaidi ya siku ya kuaga mwili bofya hapa

8 comments:

Anonymous said...

Beautiful family! May his soul rest in peace

Anonymous said...

Jamani miaka thelathini huna mawasiliano na ndugu zako nyumbani? kwa sisi tunaoishi nje ata kama tumeanza familia na watu ambao siyo watz tujaribu kuwaunganisha na watu wa nyumbani Ili taarifa kama hizi wazipate.

Anonymous said...

Miaka 30 bila kuwasiliana na ndugu zako?????? Inawezekana kweli???? Hasa hata hao ndugu wakipatikana leo, ndio wafanyeje sasa?

Anonymous said...

May God Rest His soul in Peace. Kwa mjumbe aliye-comment kwanza assuming kwamba Mike alitelekeza ndugu zake ndio maana hawajulikani nk...its an unfair judgment to a dead soul! Humjui Mike vile family yake Africa, na hasa Hapa Marekani na Jumuia yake aliyoishi nayo hapa Marekani kwa zaidi ya Miaka 30 na kuweza kumfahamu!Ni Makosa kufanya hivyo kwani huna hakika na maoni yako. Hili ni Tangazo la Kifo kama vile Matangazo ya vifo ktk redio ya taifa Tz or redio One etc!The difference is how matngazo ya hapa na huko huwekwa ktk vyombo vya habari. And if at all presuming you were right, hujui situation ya mahusiano yake na family yake Tanzania hadi yeye kuishi Marekani bila mawasiliano. Its easy to fall into stereo types without any merit ndugu Mtanzania!
May God Bless Mike's soul and Give familia yake nguvu za imani ktk kipindi hiki cha majonzi AMEN!

Anonymous said...

Uraia pacha!!!

Anonymous said...

Wee anony wa 4: NOTHING YOU SAID MADE SENSE. Ukweli upo pale pale, kuwa haingii akilini kwa mtanzania kukaa na mke na watoto over 30yrs na hajawapeleka nyumbani au hata kumpa namba za simu huyo mke mtoka mbali just in case of emergency hawa ni ndugu zangu, na watu tujue kusamehe, no matter what the situation was ITS OUR RESPONSIBILITY TO REMEMBER KUWA SISI SI MIUNGU ONR DAY PUMZI ITAZIBA NA HUTOWEZA KUJITETEA KWA LOLOTE LILE THAN HAO WALIOBAKI. Hivyo ndugu zangu nawakumbusha kuwa sisi ni watanzania kwanza na ni wajibu wetu kuunganisha familia zetu huku majuu na kule nyumbani kuna SKYPE, WHATSUP, MESSENGER, FACE TO FACE YOU NAME IT. Kama huwezi kwenda hata TEXT???? SIMU???? Maana huyo mkewe hajui shemeji, mawifi wala wakwe???? ITS COMPLETELY STRANGE, lazima tukubali ukweli na tutumie huu msiba kuanza kuishi RESPONSIBLY!!!! Hawa watoto ndo WAMEKWINET HATA BONGO HAWAIJUI NA SASA NDO KABISA HAWATAIJUA, angalia tumepoteza wabongo 4!!!! Hata wale waliokuja huku kwa ukimbizi wanawasiliana na ndugu zao bongo.

Anonymous said...

Please people acheni maneno si ajabu alikua anawasiliana na ndugu zake but hawa watu weusi ukiwa unawasiliana na ndugu sio watu wa kusema hebu nipe simu niongee na ndugu yako. Kama hajamuona, ndugu yako ni ndugu yako na sio kuwa ni hawapendi ndugu zako but they don't have that oh my sister in law is my friend...this and that....

Halafu kwao ndugu ni baba, mama, kaka na dada wengine ni watu wa mbali sana sasa ukiona wanavyosema wazazi wa huyu mtu walishafariki na haijulikani kuwa alikua na kaka na dada.

The only thing I don't know why is that hakuwa na mawasiliano na huyo waliosema ni ndugu yake yupo Minnesota. Wisconsin na Minnesota sio mbali ila ya ndugu hatuyajui but sio kuwa watu wanajisahau ni kuwa ukioa watu wenye culture nyingine ndio hivyo and especially wanaume you have to force them to home..

Anonymous said...

Hili ni swala la sisi sote ambao tupo mbali na ndugu zetu mbali na tulupo tuwape contact rafiki zetu wa karibu iwapo jambo limetokea nilahisi kujua ndugu zako na kufikisha taarifa kwa wanaohusika.
Kwani hata leo hii Wabongo wengi tupo hapa USA tunakula pamoja lakini hatujawahi kupeana contact za nyumbani kwa rafiki zetu tuliokuwa nao kila siku.