ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 26, 2014

MPE UHURU MPENZI WAKO AKUPE RAHA


Si kila mwanaume anajua maana ya kupendwa, wengine huona kufanya baadhi ya vitu ni usumbufu. Kwa mfano kuoshwa, kulishwa, kufanyiwa usafi wa sehemu nyeti, kuvuliwa nguo kubebwa mgongoni wanaume wengi huona usumbufu na hii hutegemea na makabila.

Jamanii, makubwa madogo yana nafuu, wakati watu wanalilia mapenzi kwa wenza wao kuna watu wanaona eti ni usumbufu.

Hii ilitokea juzi baada ya mtu na mkewe kunifuata, niliyoyasikia nilibakia kinywa wazi. Lakini baada ya kulifanyia kazi nilipata jibu kuwa huwezi kufanya mtihani bila kusoma maswali uliyoulizwa ni wazi utafeli.

Mtoto wa Kitanga kaolewa na mwanaume toka Bara, mtoto ili kuongeza upendo kwa mume aliyafanya yote aliyopitia kwenye unyago ili mwanaume ajue kampata mwanamke kwenye sirika ya kike, siyo mwanamke maumbile lakini tabia hata za kiume hana.

Unanishangaa nini? Ukweli ni huo, uchukie, ulie mi simo shida yangu uinywe japo chungu lakini ndiyo tiba yako. He! Nimeingia kwenye mada isiyonihusu hebu tuendelee na yetu. Basi mwari kila alilokuwa akilifanya kwa mumewe ilikuwa kama usumbufu.

Akiambiwa panda mgongoni mwanaume wa watu anaona aibu, kukatwa kucha hataki na kuogeshwa hataki.Unajua utaona utani lakini kuna wanaume hata kuoga na wake zao huona aibu, uongo? Unamwangalia nini mkeo?

Nazunguza na wewe, jamani mahaba yana nguzo zake kuna mambo yanataka uyajue mapema ukifanyiwa usishangae. Mmh! Nimekumbuka kuna siku katika pitapita yangu enzi zile niliangukia mikononi kwa mwanaume mmoja toka

Bara, jamani mbona aibu kila nilichomfanyia kwake ilikuwa karaha yeye yalichojua katika mapenzi ni kumdandia mwanamke na kumwaga mzigo kisha kuondoka hata maandalizi hajui.
Jamani mi siwacheki kwa vile ndivyo walivyolelewa, wengi mapenzi wameyaanzia ukubwani.

Usifikiri ‘mashikolo mageni’ ni kwenye chakula tu hata kwenye mapenzi. Ukitumia mdomo anaruka anaona kama unataka kumtafuna jamaniii! Mmh mbona kazi. Usicheke inatia huruma watu hawa wanatakiwa kufundwa taratibu na mwisho wake watazoea na kujua kumbe mapenzi mpaka tendo la mwisho la kukutana kimwili yanapitia njia nyingi.

Basi baada ya kuyakumbuka yangu yaliyofanana na mwari wangu ambaye alikosa uhuru wa kuonesha aliyofundwa jinsi na kumfanya mwanaume apagawe, niliwaweka chini na kutoa mafunzo ambayo na wewe tega sikio hasa wewe wa Bara uliyezoea kupanda juu ya mnazi na kuangusha nazi kisha unateremka.

Jamani vitu hivi kwetu Pwani ni jambo la kawaida ambalo naimani linaweza kuwa limesambaa nchi nzima.
Jamani shoga zangu nafasi ni finyu tutaendelea wiki ijayo.
Mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu.

GPL

No comments: