Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Dr Mary Nagu(katikati) na mkuu wa kitengo cha biashara za benki cha benki ya NMB, Filbert Mponzi wakati wa uzinduzi wa mpango wa uwezeshwaji kwa madereva wa bodaboda wa mkoa Mwanza. Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Tilapia ya jijini Mwanza.
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Dr Mary Nagu akipeana mkono na mkuu wa mkoa wa Geita Saidi Magalula wakati wa uzinduzi wa mpango wa uwezeshwaji kwa madereva wa bodaboda wa mkoa Mwanza. Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Tilapia ya jijini Mwanza
Waziri wa nchi ofisi ya waziri mkuu uwekezaji na uwezeshwaji, Dr Mary Nagu akipeana mkono na meneja mkuu wa kampuni ya Quality Motors Madhusudan Se3shadri wakati wa uzinduzi wa mpango wa uwezeshwaji kwa madereva wa bodaboda wa mkoa Mwanza. Uzinduzi huo ulifanyika katika hoteli ya Tilapia ya jijini Mwanza.•Ni mikopo kwa ajili ya pikipiki za miguu miwili na mitatu
Mwanza, Machi 10, 2014….Benki ya NMB kwa kushirikiana na Fair Deal Auto Private Ltd, Car & General Limited Ltd pamoja na Quality Motors yawawezesha wananchi kupata mikopo nafuu ya kumiliki pikipiki za miguu miwili na mitatu.
Hii yote ni katika kuendeleza azma ya NMB inayolenga kubuni huduma na bidhaa mbali mbali za kibenki zinazogusa kwa karibu mahitaji ya wateja na watanzania kwa ujumla.
Kwa kutambua hili, benki ya NMB kwa kushirikiana na kampuni ya Fair Deal Auto Private Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu na miwili aina ya Bajaj, kampuni ya Car & General Limited Ltd inayosambaza pikipiki za miguu mitatu aina ya TV’S King pamoja na kampuni ya Quality Motors wao wanasambaza pikipiki za miguu miwili aina ya Honda zimeingia ubia ili kuwawezesha wananchi kupata mikopo nafuu.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa mikopo hii, Waziri wa Uwezeshaji na Uwekezaji kutoka ofisi ya Waziri Mkuu, Mhe. Mary Nagu amesema mikopo hii inaonyesha ni jinsi gani NMB imekua kipaumbele katika kuleta bidhaa zinazomuwezesha Mtanzania hasa vijana kujikimu kiuchumi kwa kuweka vigezo na masharti nafuu kwa mkopaji.
“Mikopo hii ya pikipiki itawasaidia sana vijana na wananchi kwa ujumla kuweza kumiliki pikipiki itakayowawezesha kuendesha maisha yao ya kila siku” Alisema Nagu, akiongeza “ Binafsi natambua ajira kwa vijana imekua ni changamoto maeneo mengi nchini hivyo basi ningependa kuwasisitiza vijana wachukue fursa hii inayotolewa na NMB kuweza kumiliki biashara zao wenyewe na kujikimu kiuchumi.”
Vilevile kutoka NMB, Mkuu wa Kitengo cha Biashara, Bw.Filbert Mponzi amesema kuwa bidhaa hii mpya ina lenga kabisa kupunguza changamoto ya ajira kwa vijana hapa nchini.
“NMB itaendlelea kubuni bidhaa ili kupambana na changamoto za kibenki zinazowakumba wateja. Pia, tutaendelea kushirikiana na makampuni kama Fair Deal Auto Private Ltd, Car & General Limited Ltd pamoja na Quality Motors ili kupata bidhaa zenye ubora zaidi.” alisema Mponzi.
Mponzi aliongezea kwamba mikopo hii yenye masharti nafuu inatolewa kwa mteja yeyote ambaye atatitimiza vigezo vilivyowekwa ili kupata mkopo huu. Anachotakiwa kufanya mteja ni kulipia asilimia thelathini ( 30%) ya bei ya pikipiki ya miguu miwili au mitatu kama inavyouzwa na wasambazaji wa pikipiki hizi za Fair Deal Auto Private Ltd , Car & General Ltd pamoja na Quality Motors.
Marejesho ya mkopo huu wa pikipiki ya miguu miwili na mitatu yanatolewa ndani ya muda wa miezi 24, ambapo kwa kipindi hiki chote, mteja ataendelea kurejesha makato yake ya kila mwezi kwa taratibu za makubaliano yatakayofanyika baina ya mteja na benki ya NMB.
Mikopo hii pia inawekewa bima kwa ajili ya ulemavu au kifo kitakachomtokea mmliki wa pikipiki iliyochukuliwa mkopo. Bima hii ni kwa ajili ya kumpa unafuu mkopaji endapo atapata matatizo ya kiafya ambayo yatamfanya apate ulemavu wa kudumu au kupoteza maisha.
Mikopo hii kwa sasa inatolewa katika matawi ishirini na moja tu nchi nzima.Na kwa hapa Mwanza matawi yetu ya Buzuruga na Kenyata Road ndio yanayo husika na mkopo huu kwa sasa. Mikakati ya benki ya NMB ni kuongeza huduma hii kwa siku za usoni ili kuwafikia wateja wa NMB katika matawi ya NMB yote. Vilevile, mikopo hii inapatikana katika matawi yetu kanda za Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Moshi na Tanga
No comments:
Post a Comment