Taarifa kuhusu wagombea Ubunge Chalinze
Jumla ya wagombea watano wamechukua fomu za kuwania Kiti cha Ubunge
katika Jimbo la Chalinze, Bagamoyo, zoezi ambalo litafungwa rasmi tarehe
12 Machi 2014 saa kumi kamili alasiri, kwa mujibu wa taarifa ya Afisa
Uchaguzi wa Jimbo la Bagamoyo, David Shija.
Wagombea hao ni:-
Wagombea hao ni:-
- Mathayo Torongey (CHADEMA)
- Phabian Skauki wa (CUF)
- Vuniru Hussein (NRA)
- Ramadhan Mgaya (ASP)
- Ridhiwani Kikwete (CCM)
Nayo taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa,
Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kwenda kwa vyombo vya habari inasomeka
ifuatavyo:-
Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa katika Kikao chake Maalum kilichofanyika trehe 09/03/2014 pamoja na mambo mengine:-
- Kilimteua Ndugu Ridhiwan Kikwete kuwa Mgombea wa CCM wa nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Chalinze katika Uchaguzi Mdogo utakaofanyika tarehe 06/04/2014.
- Uzinduzi wa Kampeni utafanywa na Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi Ndugu Abdulrahman Kinana na kufungwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar) Dr. Ali Mohamed Shein.
- Kampeni zitaendeshwa na Chama ngazi husika na kuratibiwa na Katibu wa NEC-Itikadi na Uenezi, Ndugu Nape Moses Nnauye.
Aidha, katika kikao hicho Kamati kuu ilipokea taarifa ya maendeleo ya
Kampeni za Uchaguzi Mdogo wa JImbo la Kalenga na kuridhika na mwenezo wa
Kampeni ambapo CCM inategemea kupata ushindi mkubwa.
Chama Cha Mapinduzi kinawatakia kampeni njema na Uchaguzi mwema wananchi
wa Jimbo la Chalinze. Vyama na Wagombea washindane kwa hoja si matusi
wala kupigana. Tuendelee kudumisha Umoja, Amani na Mshikamano wetu.
No comments:
Post a Comment