ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 12, 2014

TAARIFA YA MSIBA NEW YORK NA TANZANIA

Kama mlivyofahamishwa awali Mtanzania mwenzetu Mama Lulu John Maro Mwaluko amefariki dunia asubuhi ya siku ya Ijumaa tarehe 7 Machi 2014. Mama Mwaluko alikuwa akikaa Queens, New York na alishawahi kuwa mwalimu na alifundisha high school hapa New York. Mama Mwaluko alifariki baada ya kuugua ugonjwa wa saratani yaani kansa. Alikuwa akitibiwa huko katika hospitali ya Calvary huko Bronx, New York.
Tunahitaji kukusanya kiasi cha 13000 us dollars kwaajiri ya kusafirisha mwili kwenda Moshi Tanzania kwa mazishi.
Familia itashukuru msaada wowote wa kuwasaidia kuweza kufanikisha mpango wa kumsafirisha mama yetu kwa kutoa chochote.

Bank: Citibank
Routing Number: 021000089
Account Number: 02472079
Bank Address: Citibank, Jamaica 89-50 164th St, Jamaica, NY 11432.
Jina la Account: Nanna Mwaluko na Helen Mwaluko.

Mama Mwaluko alishawahi kukaa na Marehemu mumewe China na Marekani kama Wanadiplomasia na alishastaafu kufundisha mwaka 2012 na kabla ya kufariki alikuwa mbioni kurejea Tanzania.

Mama Mwaluko atakumbukwa na familia yake kama mama, dada, shangazi, mwalimu, mcha Mungu na mama mwenye busara. Katika kuomboleza msiba wa Mama Mwaluko, Watanzania wote tunaombwa kuifariji familia yake na ndugu zake kwa kujumuika nao katika sala na michango katika wakati huu mgumu wa maombolezo. Mnaweza kuwasiliana na Emma Kasiga kwa simu namba +1612-229-4050 na Nanna Mwaluko kwa simu namba +1347-693-6129 na Camelot Funeral Home kwa simu namba +1914-664-8500. Kwa yeyote anaetaka kutoa alichonacho unaweza kupitia Ubalozi wa Tanzania hapa New York  Ubalozi utakuwa wazi hadi saa 12 jioni Address hii. Msiba huu ni wa Watanzania wote tushirikiane hili kufanisha safari ya misho ya marehemu.

Tanzania Mission to the UN
307 East 53rd Street, 4th Floor
New York, NY 10022
Tel: 201-252-7220

Siku ya Jumatano itakuwa ni siku ya kuaga mwili wa Marehemu kuanzia saa tisa na nusu hadi saa mbili za usiku pale Camelot Funeral Home. Anwani ni: Camelot Funeral Home, 174 Stephens Avenue, Mount Vernon, New York, 10550. Wote mnaombwa kufika kumuaga Mama Lulu John Maro Mwaluko na kuifajiri familia yake.

Imetolewa na Uongozi - Jumuiya ya Watanzania New York.

Mwenyezi Mungu aiweke roho ya Marehemu mahali pema peponi. Amina.

3 comments:

Anonymous said...

Dj Luke nashauri tu, may be ukiandika tel. mamba uweke na code, my be kuna wengine watataka kupiga kutoka nje ya USA. ushauri tu. Thanx.

Anonymous said...

code ya kupiga USA si huwa ni 1 au imebadilika? au mwenzetu mgeni wa kupiga simu USA?

Poleni wafiwa, RIP mama aunt Lulu

Mande P. said...

Hilo ni wazo zuri sana la mchangiaji hapo juu ila wewe uliyecoment hapo unaonekana unatatizo la uelewa tu,maana usifikiri kila unayemuona anajua jibu la 0 -2 ni ngapi elewa namna yamkudeal na watu sio na mtu,,hongera kwa kuijua sana marekani.Luke,hongera kwa kazi fanyia kazi ushauri huo,Wafiwa Mungu awafarji kwa neema yake iliyokuu.