Advertisements

Thursday, April 24, 2014

TAARIFA YA UCHAGUZI MKUU - JUMUIYA YA WATANZANIA WASHINGTON DC, MARYLAND NA VIRGINIA


Uongozi wa Jumuiya ya Watanzania DMV unawataarifu kwamba uchaguzi wa Kuwachagua viongozi wa Jumuiya , utafanyika kati ya Mwezi wa mwishoni mwa mwezi wa wa tano au mwezi wa 6. Tarehe Rasmi ya Uchaguzi itatangazwa na kamati ya uchaguzi ambayo imeshachaguliwa na Bodi.

Katiba ya jumuiya inashurutisha kwamba ni Wanachama Hai Tu ambao wamelipa michango ya mwaka wanaoweza kuchagua Viongozi na Ni wanachama hai tu watakao weza Kuchaguliwa  kuwa Viongozi.  

Katiba inaelekeza kuwa wagombea na wachaguaji wanatakiwa wawe wamelipa mchango wote wa mwaka siku 30 kabla ya Uchaguzi. Kwa maelezo zaidi soma katiba hapa.

www.watanzaniadmv.org/about.asp

Nafasi zitakazogombaniwa ni :

1. Rais
2. Makamu wa Rais
3. Katibu
4. Makamu wa Katibu
5. Muweka Hazina
6. Makamu wa Muweka Hazina

Mungu Ibariki Jumuiya ya Watanzania DMV
Imetolewa na Uongozi
http://www.watanzaniadmv.org/