ANGALIA LIVE NEWS

Monday, March 3, 2014

UNAAMBIWA WASTARA ASUMBULIWA NA ROHO YA KIFO

Wastara Juma.Stori: Gladness Mallya na Hamida Hassan
OOOH! Zikiwa zimepita siku chache tangu staa wa filamu Bongo, Wastara Juma kunusurika kifo baada ya kudaiwa kunywa sumu na baadaye kupata ajali, anadaiwa kusumbuliwa na roho wa kifo.
Kupitia ukurasa wake katika Mtandao wa Kijamii wa Instagram, Wastara aliweka picha za wasanii mbalimbali huku akimwelezea kila mmoja alivyo na mwishoni mwa maelezo hayo alimalizia kwa kusema kuwa ameamua kusema kabla hajafa kwani kifo hakiko mbali.
00Baadhi ya mastaa aliowaelezea ni Tamrina Poshi ‘Amanda’, Denis Swea ‘Dino’, Jacob Steven ‘JB’, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’, Halima Yahya ‘Davina’, Riyama Ally, Salma Jabu ‘Nisha’.
Wengine ni Cloud, Lamata, Bondi, Msafiri Kondo na wengineo ambapo baada ya kumuelezea kila mmoja, chini alikuwa akiandika ujumbe huu:
“Sababu ya kufanya hivi, sisi ni binadamu na kifo hakiko mbali, naweza nikafa kabla sijasema lolote kwa watu wangu.”
WASTARA ANASEMAJE?
“Niliandika maneno hayo ili wasanii wote waliowahi kunitendea wema wajue kwamba wao ni watu muhimu sana katika maisha yangu, wapo wengi lakini sikuweza kuwashukuru wote kwa sababu wakati naandika hivyo nilikuwa kwenye hali mbaya sana.
“Unajua siku moja nitakufa maana kifo kiko karibu sana hivyo watakumbuka maneno yangu hayo niliyoandika ya kuwashukuru,” alisema Wastara.
Baada ya kuwaelezea kwa kuwaandikia waraka huo, mashabiki mbalimbali waliopo kwenye mtandao huo walionekana kusikitishwa na maneno hayo na kujikuta wakimuuliza maswali yasiyokuwa na majibu kwa wakati huo huku wengine wakidai kuwa Wastara anasumbuliwa na roho wa kifo.

4 comments:

Anonymous said...

Hakuna cha roho ya kifo, hizo ni imani duni za watu wasiopenda kufikiri na kuwahusisha wataalamu.Kimtizamo utaona quite obvious huyu dada yuko depressed. Hivyo anatakiwa kuwaaona madokta, ma pychologists waweze kumsaidia.Uswahili anapaswa kuweka pembeni.

Anonymous said...

Hii ni depression. Asaidiwe asije akajiua. Tanzania bado kabisa kumbe. Mpelekeni apate utaalamu wa kipsychologia na hata dawa zipo. Watamwachia ajiue tu halafu watasema kalogwa. Dawa zipo za depression waambieni ndugu zake wampeleke.

Halima Senkukus said...

Mh! Tanzania niijuayo mimi, si ile niliyoiacha miaka 2 iliyopita. Uchawi upo but kwa hili la huyu mwanamke mwenzangu si kulogwa, jamani wanachi wenzangu wa Tanzani tuamke. Huyu anahitaji mwanasaikologia atakae msaidia, tatizo walikuwa wawili na sasa mmoja ametangulia mbele ya haki na anajiona mpweke na hakuna wakupeana mawazo kama walipokuwa wawili. Walio karibu na huyu dada ningewaomba wamkimbie hospital haraka before hajajimaliza. Shame on us, kila anaepatwa na jambo baya amelogwa. Uliweza ulikuwa jasiri kipindi cha mtihani mkubwa wa mumweo, basi naomba akubaliane na ushauri wa watu wa hekima kumshauri kwenda kumuona mwanasaikologia. Depression ni mbaya it's not a joke. 2

Anonymous said...

Nenda kafanyiwe maombi Dada.