ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, March 20, 2014

VAN PERSIE AINUSURU MAN UNITED

Robin van Persie asherekea kufunga mabao matatu.


Robin van Persie alifunga mabao matatu na kuisaidia mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Uingereza Manchester United, kujikatia tiketi ya kushiriki robo fainali ya kombe la kilabu bingwa barani Ulaya baada ya kuinyuka Olympiakos mabao 3-0 katika mechi ya mkondo wa pili iliyochezwa Old Trafford.

Van Persie alifunga mkwaju wa penalti baada ya kuchezewa vibaya mda mchache tu kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.
Van Persie asherekea na Rooney.


Baadaye mshambulizi huyo wa Uholanzi aliongeza bao lingine baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa mshambulizi mwenza Wayne Rooney.

Van Persie alifunga bao lake la tatu kwa mkwaju wa free kick na kumhakikishia Moyes fursa ya kujiunga na Chelsea katika hatua ya robo fainali ya mchuano huo wenye kitita kikubwa zaidi barani Uropa.
Licha ya mashambulizi kadhaa Olympiacos kutoka Ugiriki mlinda lango wa Manchester United David De Gea alilazimika kufanya kazi ya ziada kuinyima klabu hiyo kutoka Ugiriki bao moja tu la ugenini

Olympiacos ilishinda mechi ya kwanza mabao 2-0 na ilihitaji sare ya aina yeyote ama bao moja tu la ugenini ilikufuzu kwa hatua ijayo kutokana na sheria ya bao la ugenini. GPL

No comments: