ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 12, 2014

VIONGOZI WA CHADEMA WILAYANI MAKETE WAPINDULIWA

  Aliyekuwa Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Makete Shaaban Mkakanze.
 

Hatua hiyo imefikiwa baada ya mkutano wa wanachama uliofanyika jumamosi machi 8, mwaka huu kwa pamoja kuazimia kuung'oa madarakani uongozi uliokuwepo baada ya kujadiliana kwa kina katika mkutano huo

Miongoni mwa viongozi waliong'olewa ni pamoja na mwenyekiti wa chama hicho wilaya ya Makete Bw. Sahaaban Mkakanze na katibu wake pamoja na uongozi mzima uliokuwa ukiongoza chama hicho wilayani.
Mkutano huo ambao pia uliowashirikisha viongozi wa chadema mkoa wa Njombe akiwemo mwenyekiti Bw. Lulandala, ulibaini kuwa kasi ya kukua kwa chama hicho wilayani Makete ni ndogo ukilinganisha na maeneo mengine licha ya jitihada zinazofanywa na ndiyo maana wakaona wabadilishe uongozi

Katika mkutano huo waliazimia kuchagua uongozi wa muda ambao umepewa miezi miwili ya matazamio kuhakikisha wanakiimarisha chama katika kata zote za wilaya ya Makete ikiwemo kuunda uongozi wa kila kata ambao unaweza kufanya kazi kama inavyotakiwa

Viongozi wa wa muda waliochaguliwa kushikilia chama hicho ngazi ya wilaya kwa muda ni Bw. Ibrahim Ngogo ambaye ni mwenyekiti, Bw. Ilomo ambaye ni katibu na Bw. Stephano Kasanga ambaye ni katibu mwenezi

Mkutano huo umewapa miezi miwili ya kukiimarisha chama kabla ya kuitishwa mkutano mwingine ambao utakuwa wa uchaguzi wa wanachama kuwachagua viongozi wa wilaya wa kukiongoza chama hicho

1 comment:

Ibrahim Ngogo said...

si kweli kwamba mwenyekiti wa wilaya mzee mkakanzi ameng'olewa, mzee mkakanzi alivyoona viongozi wenzake wananunuliwa nunuliwa na ccm akaamua kuuomba uongozi wa chama ngazi ya mkoa kuongezewa nguvu ili chama kiweze kusonga mbele. mimi kama mwenyekiti mpya nafanya kazi na mzee mkakaknzi pamoja na ndie alipewa ungalizi wa karibu katika kutusukuma na kutuonyesha njia takatifu katika kukijenga chama makete. namshukuru mzee mkakanzi kwa kukitoa chama mahali kilipokuwa na kukiweka hapa kilipo, na mimim kama mwenyekiti wa muda nafanya kazi kwa kupewa ushauri na mzee mkakanzi kwa karibu sana, ila nawashauri vyombo vya habari mnavyotoa habari muwe mnatangulia kuhoji sehemu zote mbili ili habari yenu isiwe ya polopaganda. hii ni sauti ya chama.