Askofu Mark walwa Malekana akiongea na waandishi wa habari ambao walifika ilala mchikichini kushuhudia waumini wakichangia damu
Afisa mwendeshaji Mpango wa Taifa wa Damu Salama Dr. Abdu Juma akimshukuru Askofu Mark walwa Malekana kwa kuhamasisha waumini wa makanisa ya sabato kujitolea damu kwa hiari kuokoa maisha ya wagonjwa
Meneja wa Damu salama kanda ya Mashariki Dr. Avelina Mgasa akimkaribisha askofu kuongea na waumini
Lengo ni kukusanya chupa 3000 katika mikoa hiyo, akiongea na waumini waliofika katika kituo cha Damu salama ilala mchikichini Askofu wa Jimbo la Mashariki ambalo linajumuisha mikoa ya Dar-es-salaam, pwani, Dodoma, Morogoro, Lindi, Mtwara na Zanzibar Mark walwa Malekana aliwashukuru waumini kwa moyo wa upendo wa kuja kuchangia damu na akawaomba waendelee na moyo huo ili wawe wachangia damu wakujirudia kwani mwanaume anaweza kuchangia mpaka mara nne kwa mwaka na mwanamke mara tatu kwa mwaka .
Askofu Mark walwa Malekana pia alikemea tabia ya baadhi ya watumishi wa hospitali ambao wanajihusisha na tabia ya kuuza damu kuwa waache tabia hiyo kwani ni dhambi watu wanajitolea kwa hiari na upendo kuchangia damu bila malipo yoyote hivyo wanapaswa kupata huduma hiyo bila Bure.



No comments:
Post a Comment