ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, March 12, 2014

WAANDISHI WANAWAKE WANAFANYA KAZI KATIKA MAZINGIRA MAGUMU-UTAFITI

 1. Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Irina Bokova,  ( kati kati) akizungumza wakati wa majadiliano kuhusu Teknolojia ya habari na mawasiliano na  mchango wa  vyombo huru vya habari katika  kuwawezesha wanawake na watoto wa kike,  katika majadiliano hayo,  wazungumzaji waliokaa meza   kuu ambao ni  kutoka  kushoto,   Bi. Elisa Munoz,  Mkurugenzi  Mtendaji wa  IWMF, Muwakilishi wa Kudumu wa Austria Balozi Martin Sjdik, Bw. Peter Launsky-Tieffenthal  Katibu Mkuu  Msaidizi  na mkuu wa Idara ya  Mawasiliano ya Umma ya Umoja wa Mataifa , Anne Bennett, Mkurugenzi Mtendaji wa Hirondelle ( USA) na Pamela S. Fall,  anayeripoti katika  kituo cha  CBS na Rais wa  chama cha Waadishi wa habari  Umoja wa  Mataifa walijadili kwa kina umuhimu wa teknolojia ya habari na mawasiliano kama nyezo muhimu ya uwezeshaji wa wanawake na watoto  wa kike, lakini pia kama  nyezo muhimu katika kuwapatia habari na taarifa mbalimbali, habari zinazoandaliwa na vyombo huru na ambavyo waandishi wake wenyewe na weledi wa matumizi ya ICT.   
 2.sehemu ya washiri wa majadiliano kuhusu  ICT ambayo yaliandaliwa kwa pamoja na  UNESCO na Uwakilishi wa Kudumu wa Austria na kufanyika sambamba na  mkutano wa 58 wa Kamisheni   kuhusu  Hali ya Wanawake. katika majadiliano hayo, Mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya  International Women's  Media Foundation, (IWMF mwenye suti nyekundu, alitoa taarifa  kuhusu uzinduzi utakaofanywa wa  ripoti ya utafiti kuhusu mazingira hatarishi wanayofanyia kazi waandishi wa habari wanawake.  Ripoti  hiyo  yenye kurasa 40  inahusu utafiti   uliofanywa kwa kuwashirikisha waandishi wa habari wanawake  1,000 kutoka duniani  kote. 
3. Katibu Mkuu, Wizara ya  Maendeleo ya Jamii,  Jinsia na Watoto, Bibi. Anna T. Maembe,  akifutilia majadiliano ambayo  yameingia siku ya pili  ya  ajenda kuu ya Mkutano wa 58 wa  Kamisheni  kuhusu Hali ya  Wanawake,  ajenda hiyo  ni  mafanikio na changamoto za utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo ya Millenia, ( MDGs) kwa wanawake na watoto wa kike. Mkutano wa  58 wa CSW ulifunguliwa siku ya   jumatatu na  Katibu  Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon. 

No comments: