ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 23, 2014

Wapinzani wacharuka

  Wadai hotuba ya Rais Jk imetangaza kuvunjika kwa Muungano
  Wasema hawako tayari kuona mawazo ya wananchi yakichakachuliwa
Kutoka kushoto: Freeman Mbowe(Chadema), Profesa Ibrahim Lipumba(CUF) na James Mbatia(NCCR - Mageuzi)

Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), unaoundwa na wajumbe wa vyama vya upinzani walio kwenye Bunge Maalum la Katiba, umeielezea hotuba ya Rais Jakaya Kikwete ya uzinduzi wa bunge hilo kuwa imetangaza kuvunjika Muungano.

Kadhalika wajumbe hao wamemkosoa Rais kuwa hakwenda kuzindua bunge hilo bali kuzindua rasimu ya CCM na kudhalilisha maoni ya wananchi kupitia Tume ya Mabadiliko ya Katiba.

Wawakilishi hao wakichambua hotuba ya Rais walisema hotuba ya juzi imeonyesha dhahiri kutangaza rasmi kuvunja Muungano baina ya Tanganyika na Zanzibar.

Wakizungumza na wanahabari mjini Dodoma, viongozi wa Ukawa walisema hawako tayari kuona mawazo ya wananchi yakichakachuliwa kwa faida ya chama tawala.

Mwenyekiti wa Ukawa, Profesa Ibrahim Lipumba alisema kuwa katika hotuba yake, Rais Kikwete alitumia muda mwingi kuweka vitisho kuhusu uanzishwaji wa muundo wa serikali tatu kuwa endapo utapitishwa, unaweza kusababisha nchi kupinduliwa na jeshi huku akitoa maelekezo ya kuwapatia Wazanzibar mamlaka zaidi ya kujitawala kama nchi inayojitegemea.

Kutokana na kauli hiyo, ni wazi kuwa Zanzibar itajitenga kutokana na yenyewe kuwa na katiba inayoitambua kama taifa linalojitegemea.

“Sisi tulitarajia kwamba Rais atakuja kutuunganisha, badala yake hotuba aliyoitoa ni ya kututenganisha na hatuwezi kukubali kutumiwa kupitisha mambo wanayoyataka CCM badala ya Rasimu ya wananchi iliyowasilishwa na Jaji Warioba,” alisema.

Alisema alichakachua takwimu za Tume ya Mabadiliko ya Katiba kuhusu watu waliotoa maoni juu ya muundo wa Muungano na alitumia takwimu zilizotolewa kwenye baadhi ya magazeti badala ya takwimu halisi za Tume.

“Tumesikitishwa na kitendo cha Rais kutumia takwimu ‘alizookota’ kwenye gazeti la … (analitaja) na kudhalilisha rasimu ya katiba ambayo yeye mwenyewe alianzisha mchakato wake,” alisema.

Alieleza kuwa badala ya kuzindua bunge hilo, alitumia muda mwingi kusisitiza msimamo wa CCM kwa kupigia debe rasimu inayodaiwa kuwa tayari imeandaliwa na chama hicho kitu ambacho hakupaswa kukifanya kama Rais wa watu wote.

Profesa Lipumba alisema kama CCM walikuwa na Rasimu yao ya Katiba, walipaswa kuitisha Mkutano Mkuu wa CCM kuijadili na siyo kuipeleka kwenye bunge hilo ambalo ni chombo muhimu cha kujadili mustakabali wa nchi.

Alisema hawatakuwa tayari kuona rasimu inayopaswa kujadiliwa ambayo inatokana na maoni ya wananchi inawekwa pembeni na badala yake inaingizwa CCM.

Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia alitahadharisha kuwa endapo CCM itaendelea kuchezea mchakato wa katiba mpya itasababisha nchi kuingia kwenye machafuko.

Alisema kuwa Rasimu ya Katiba iliyopatikana imetokana na maridhiano ya Wazanzibar ambao waliunda serikali ya kitaifa, hivyo kutokana na matamko ya Rais Kikwete ni dhahiri kuwa amewatukana Watanzania kutokana na mawazo waliyoyatoa kwenye tume.

Mbatia alisema Rais Kikwete wakati akipokea rasimu ya kwanza na ya pili pamoja na kwenye mkutano wa maridhiano na vyama vya kisiasa, aliwataka viongozi wa kisiasa kuzingatia maslahi ya nchi badala ya kuweka mbele itikadi zao za kisiasa katika kuhakikisha Tanzania inapata katiba bora.

Lakini cha kusikitisha ni kwamba Rais Kikwete mwenyewe amekiuka makubaliano hayo na kuingiza itikadi yake kwa kutetea hadharani msimamo wa CCM na kupuuza maoni ya wananchi.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe alisema kutokana na hotuba yake, Rais Kikwete ameweka misingi mibaya ya upatikanaji wa katiba nzuri kwa kubeza maoni ya Watanzania.

Mbowe alitolea mfano kwa Mwanasheria Mkuu Mstaafu wa Kenya, Seneta Amos Wako aliyesema serikali iliingilia na kuchakachua rasimu ya katiba kwa kuingiza vifungu 13 ambavyo vilisababisha machafuko nchini humo.

“Rais na Chama chake cha CCM wasijidanganye kuwa wingi wao utawasaidia kuchakachua rasimu na kupuuza maoni ya wananchi, tutapambana ndani na nje ya bunge ili wananchi waweze kutendewa haki,” alisema Mbowe.

Tundu Lissu kwa upande wake alisema licha ya kanuni walizopitisha kukataza Rais asifanyiwe dhihaka, itabidi kanuni hiyo isitumike kwa kuwa Rais mwenyewe ameanza kuwadhihaki wabunge na wananchi .
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

8 comments:

Anonymous said...

Acheni uvivu,chukulieni ushauri wa Raisi kama changamoto ktk kujadili swala hili muhimu.Haingiii akilini kama mlidhani mnalipwa hela zote hizo ili kwenda kubariki rasimu ya mzee Warioba kama ilivyo.Hio haijawahi kutokea sehemu yoyote duniani.
Changamoto alizozitoa Raisi hazina tofauti na zozote zile ambazo mjumbe wa bunge hili anaweza kuzitoa na kustahili kujadiliwa.
Na vilevile inawezekana ikafika sehemu ikabidi rasimu ifanyiwe amendment ili kutoa majawabu ya concerns zilizopo.Kazi yenu ni kujadili hoja kwa vigezo hai ili tupate katiba nzuri na sio kushindana baina ya serikali 1,2,3 au 10.

Anonymous said...

Mimi nashauri waheshimiwa hawa waache siasa za mipaasho na kuwa serious katika kujadili hoja nasio personalities or kuvutia their party's interests.Vile vile kilichotokea Kenya sio lazima ki apply Tz 100%.hasa tukizingatia sisi tuna swala la muungano ambalo ndio kiini cha hizi complications zote.

Anonymous said...

jamani huko kwetu (Tanzania)ni kweli kuna wapinzani?









Anonymous said...

Hotuba wote tumeisikia na bado ipo kwenye mitandao. Hawa wapinzani watu wa ajabu kweli. Wanatudhalilisha. The President was clear and concise.

Ameeleza athari zote za aina ya Serikali tatu ama mbili. Amesema zifikiriwe athari hizo na zitafutiwe majibu. Sasa muungano wapi kutangaza kuuvunja?

See when you have an opposition whose bankruptcy has been exposed all you secure is empty rhetoric and threats.

Waelewe wananchi sio wajinga miadi hicho. Jamani Myonge myongeni lakini haki yake mpeni! Kumlaumu Kikwete kwa hotuba yake ni wongo.

Jibuni hoja. Kama alivyosema. Argue. Don't shout.

Anonymous said...

It is sad that the Professor has joined hands with empty heads!! What a pity!

Anonymous said...

Miaka hamsini 54 sasa hakuna chochote zaidi ya longolongo na ufujaji wa pesa za kodi za wananchi tumechoshwa na chama tawala tunataka cha kingine vitishi vingi tumechoka sasa kimekuwa chama cha watawala na watoto wao wanarithishana tu yani hii ni aibu tokeni madarakani tujaribu na chama kingine tuone mabadiliko.

Mtanzania, Washington,DC said...

Lipumba, Mbowe, and Mbatia combined represents, barely 25% of Tanzanian youths (The major voting block). With such a luckster number, whose interests are they really representing? Just as a reminder to these three confused opposition leaders, the fact is: Tanzanians who will be most impacted by the outcomes from Dodoma are the approximately 20-30 million youths out of an estimated population of 49 million. If the three of you command merely 25%, then mathematically, your share of youth followers is around 6.25 million (the majority of whom are ineligible to vote). Your taunts that you represent "Wananchi", is self-defeating. The majority of Tanzanians applauds the president's speech, except the pity three of you!

Anonymous said...

I agree with the opposition on this one. Citizens have spoken. Lets all learn how to be open and have a honest discussion. Its not because our President said something, then that should be like a blue print going forward. I'm challenging CCM too on this one.