ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, March 30, 2014

WATANZANIA WENZETU WAMEZUIA KUCHOMWA MOTO KWA MPENDWA WETU MIKE LUKINDO MADISON, WISCONSIN

Watanzania Wisconsin wamezuia kuchomwa moto kwa mpendwa wetu Michael Lukindo aliyefariki Jumapili ya March 16, 2014 wameomba msaada kwa Watanzania wengine waishio Marekani na kokote pale Duniani kujitahidi kadri tuwezavyo tuweze kumstiri Mtanzania mwenzetu ghrama za mazishi ni $6,000 
jina la AC ni Memorial for late Mike Lukindo 
Benki ni Madison Chase Bank AC ni 579362299 
Route ni 075000019 
Tafadhali ndugu zangu, Watanzania wenzangu msiba huu ni wetu sote chochote utakachokua nacho kitasaidia kumzika ndungu yetu asante

8 comments:

Anonymous said...

Poleni wafiwa hapa na Tanzania . Mungu awape uvumilivu katika kipindi hiki kigumu. Naomba nitoe maoni yangu: nadhani ni wakati muafaka wa kuanza kuambiana ukweli. Kwa Wabongo tunaoishi nje kama Una karatasi la nchi yeyote ile unayoishi PLEASE GET LIFE INSURANCE ZIPO CHEAP ONES HADI ZA DOLA $30 KWA MWEZI NA kama huna karatasi sasa kuna WESTADI! Wazungu wanasema "you learn from your past mistakes". What have we learned from past year????? Hasa hapa Marekani?? Watanzania wangapi wamefariki na ikabidi kufanya harambee?? au kuitisha michango huku online halafu baada ya misiba tunasikia watu wanagombana sababu ni kurushana au kutapeliana hizo hela za watu waliotoa kwa kuona imani ya wafiwa. Lazima tukubali kuwa kila mtu ipo siku utaondoka swali ni kujiuliza umejitayarishaje wewe na familia yako??????

Anonymous said...

Suali kwa anonymous wa juu hapo, kwani LIFE INSURANCE ni kwa ajili ya maziko au ya jamaa zako kuwaachilia hela ya urithi kwani hio pesa ya LIFE INSURANCE sio kama unaipata hapopapo ila kuna prosses lazima ufuatilie.

Anonymous said...

Amekaa miaka yote hiyo kwani hana hata saving account halafu mbaya zaidialikatata mawasiliano kbs na familia yake ya tanzania mwenyezi hamsamehe but shame .

Anonymous said...

JIBU. ..LIFE insurance ni kwa ajili ya gharama za maziko na madeni mengine yaliyoachwa na marehemu kama gharama za hospital! ! Kilicho baking ndiyo unapewa mfiwa...Ni kweli hatujifunzi life insurance ni very cheap! Hakuna haja ya kuchangishana hela za maziko au usafirishaji wa maiti.Life insurance inatoka haraka sana bila kuchelewa na bila usumbufu wowote hapa USA.

Anonymous said...

Research and you will find there are so many different kind of insurance for different purpose nyingine inaweza ukawa unatoa hela wakati bado unaishi. Ila this is not the forum to discuss. Labda viongozi wetu wa jumuia walifuatilie ili jambo na kuhamasisha wakazi wa huku nje.

Anonymous said...

Moja ya mafao ya Term Life Insurance ni pamoja na kugharimia gharama za mazishi/funeral costs na kama umekata kwenye kampuni inayoeleweka hiyo hela inatoka immediately baada ya kuonyesha cheti cha kifo/death certificate. Kwa hiyo ni wazo sahihi kabisa kwa mtoa hoja wa kwanza. Unaweza hata kukata term life insurance ya $10 kwa mwezi. Watanzania iwe nyumbani au ughaibuni inabidi kujifunza kuwa ni muhimu kupangilia mambo baada ya maidha hapa duniani badala ya kila mtu kusema watajua watakao kuwa wamebaki, hili ni jamabo la aibu kwa kila litakaye mgusa kama hujajianadaa.

Anonymous said...

yeye katangulia nasie nyuma yake tutafuatia.Marehemu kwa hadithi za hapa na pale yuko hapa Marekani tangu miaka ya 80 kama sikosei.hakujishirikisha na watanzania wenzake wala ndugu na jamaa zake.na kuchomwa ni matakwa ya mtu ukiwa hai unaweza kuandika kwenye will yako kuwa unataka ufanyiwe hivyo.SWALI LA NYIE MNAOZUIA ASICHOMWE , KWANINI MNAOMBA MSAADA?CHANGENI MAPESA ILI AKAZIKWE.WATANZANIA WENZANGU.NUNUA LIFE INSURANCE USIWAPE FAMILIA YAKO MATATIZO PINDI UTAKAPOPATWA NA MAUTI.NAKAMA UNAONA KUJUMUIKA NA WATANZANIA WENZAKO SUMU BASI JIANDAE KIKAMILIFU.NA SASA TUNAZIKANA WANYEWE KWA WENYE KILA KUKICHA FINALLY HIYO WATU TULIKUJA HUKU TUKIWA VIJANA MUDA USHAYOYOMA.NUNUA BIMA YA MAISHA YAKO.

Anonymous said...

This is no accusation to our departed fellow Tanzanian, lakini kwa wale tulioachwa lazima tuukubali ukweli huu japokuwa ni mchungu. Anonymous wa kwanza ametoa hoja ya msingi sana; life insurance and what not!!! kama marehemu angekuwa na life insurance familia yake ingeweza hata kuiweka rehani hiyo policy ili kupata pesa ya kumzika mpendwa wao. Pia WESTADI, bima inayoeleweka kwa kushughulikia matatizo kama haya inagharimu less than $30 kwa mwezi.

Wakati tukifanya juhudi za kuhakikisha mwenzetu anazikwa kwa mila na desturi zetu, tuichukulie changamoto hii kama learning moment.