Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John M.
Haule (kushoto) akiwa pamoja na Balozi wa Jamhuri ya Watu wa China
nchini Tanzania, Mhe. Lu Youqing wakati wa mkutano na
waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari maelezo
siku ya Jumanne tarehe 25 Machi, 2014. Mkutano huo ulizungumzia
maadhimisho ya miaka 50 ya ushirikiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania
na China na mafanikio ya ziara ya Rais wa China aliyoifanya nchini
ambayo imetimiza mwaka mmoja.
|
Sehemu ya waandishi wa habari walioshiriki mkutano wa waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari maelezo. |
Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bibi Mindi Kasiga akisikiliza kwa makini hotuba zilizokuwa zikitolewa. wengine ni maafisa wa Ubalozi China. |
Baadhi ya maafisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje walioshiriki mkutano huo. |
Picha ya pamoja, kutoka kulia ni Balozi wa China, Mhe. Lu Youqing; Katibu Mkuu, Bw. John M. Haule; Mkurugenzi Msaidizi katika Wizara ya Mambo ya Nje, Bw. Nathaniel
D. Kaaya; Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini katika Wizara ya
Mambo ya Nje, Bibi Mindi Kasiga na Afisa kutoka Ubalozi wa China. KUSOMA HOTUBA YA KATIBU MKUU WA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA BOFYA HAPA |
No comments:
Post a Comment