Advertisements

Sunday, April 20, 2014

AZAM FC WALIVYOKABIDHIWA KOMBE LAO

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) akimkabidhi Kombe la ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, nahodha wa Azam FC, John Bocco jana jioni baada ya kuifunga JKT Ruvu bao 1-0 katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar.
Azam FC wakishangilia ubingwa wao.
Shampeni zikifunguliwa baada ya kukabidhiwa kombe.
Na Sultani Kipingo
Mabingwa wapya wa Tanzania, Azam FC, wametawazwa rasmi na kukabidhiwa kombe lao na Rais wa TFF, Jamal Malinzi, katika uwanja wa Azam Complex huko Chamazi, Dar es salaam jana.

Hii ni baada ya Azam FC kucheza mechi yao ya mwisho na JKT Ruvu na kuifunga timu hiyo bao 1-0.

Mshambuliaji kutoka Uganda, Bryan Umonyi, ndiye alifunga bao hilo baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Kipre Tchetche. Watu wengi walijazana uwanjani hapo kushuhudia pambano hilo ambalo halikuwa na kiingilio. Vikundi mbalimbali wakiwemo Wanaume TMK walioongozwa na Mheshimiwa Temba vilitoa burudani.

No comments: