ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 15, 2014

BABA WA MAPACHA SITA AFARIKI DUNIA AKICHEZA NA WANAE


Mfanyakazi wa kanisa la Calvary Baptist la Holland nchini Marekani aitwaye Ben Van Houten amefariki dunia ghafla akiwa anacheza na watoto wake baada ya kushikwa na mshtuko wa moyo. Ben ambaye ni dikoni wa kanisa hilo la Baptist hupenda kucheza na
watoto wake sita ambao ni mapacha aliopata kwa mkupuo ambao kwa neema ya Mungu mpaka leo bado wanaishi wakiwa na umri wa miaka 10 pamoja na dada yao mwenye umri wa miaka saba.
Kwa mujibu wa mtumishi mwingine wa kanisa aitwaye Louie Schaap ameiambia told Wood TV8 kwamba alizungumza na marehemu jumapili iliyopita akisema kwamba siku hiyo ilikuwa siku nzuri sana na kwamba alikuwa anasubiri kwa hamu majira ya kiangazi(summer) ili afurahi na familia yake kwa matembezi. Ambapo kutokana na kifo chake kanisa lake pamoja na kampeni ya youcaring wanatafuta dola elfu kumi za Marekani (10,000) ili kumsaidia mkewe marehemu aitwaye Amy ili kulea watoto hao saba ambao Mungu ameijalia familia hiyo, familia ambayo pia imekuwa mfano kwa marehemu na mkewe kusaidiana na kuilea familia kwa kipindi chote hicho.

No comments: