ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 14, 2014

BABU NA MJUKUU WAKE WAFANIKIWA KUINGIA HATUA YA TATU KATIKA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS

Washiriki wa Shindano la Tanzania Movie Talents ambao ni babu na mjukuu wake kiuhalisia wakipongezana mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu ya kutafuta washiriki 15 bora na hatimaye kupatikana washindi watatu bora wa kanda ya kati ambapo kila mmoja ataondoka na kitita cha shilingi laki tano za kitanzania.
Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents akihojiwa na Msanii Joti mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu hapo kesho huku mjukuu wake pia akifanikiwa kuingia hatua hiyo pia.
Washiriki wa Shindano la kusaka vipaji vya Uigizaji Tanzania lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents wakiwa kwenye mazoezi wakati walipokabidhiwa muswada (script) kwaajili ya kuifanyia mazoezi na kwenda kuonyesha uwezo wao kwa majaji.

Msanii wa Vichekesho Joti akihojiana na Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents mara baada ya kutoka kwa majaji, shindano limeingia hatua ya pili leo kwa kuchagua washiriki 30 ambao watatafutwa washiriki 15 bora hapo kesho.
Mshiriki namba 00554 akihojiwa na msanii Joti mara baada ya kufanikiwa kuingia hatua ya tatu hapo kesho ambapo watapatikana washindi kumi na tano bora na hatimaye kupata washindi watatu bora wa kanda ya kati ambapo kila mmoja atajinyakulia kitita cha shilingi laki tano za kitanzania
 
Baadhi ya washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents wakibadilishana mawazo mara baada ya kupatikana kwa washiriki 30 ambao wataendelea na mashindano hapo kesho kwaajili ya kupata washiriki 15 bora.
 Mmoja wa washiriki wa shindano la Tanzania Movie Talents akiwa amenyongonyea mara baada ya safari yake katika mashindano kuishia leo kutokana na kukosa nafasi ya kuingia katika hatua ya tatu hapo kesho.Picha na Josephat Lukaza wa Proin Promotions - Dodoma

Na Josephat Lukaza wa Proin Promotions Limited - Dodoma
Leo Shindano la Tanzania Movie Talents limeingia ya hatua ya pili ya mchujo ambapo washiriki 30 wameweza kupatikana kwaajili ya kuendelea na shindano hilo hapo kesho ambapo washiriki 15 ndio watachukuliwa kwaajili ya kuendelea na mashindano hayo na hatimaye kupatika washindi watatu bora ambao watawakilisha kanda ya Kati na kwa kila mshindi mmoja kuibuka na kitita cha shilingi laki tano (500,000/=).
Mpaka sasa washiriki 30 wameshapatikana kwa kanda ya Kati na hatimaye kesho washindi watatu watapatikana na kuiwakilisha kanda ya Kati katika fainali kubwa itakayofanyika Mkoani Dar Es Salaam na hatimaye mshindi katika fainali hiyo kujinyakulia kitita cha Shilingi Milioni 50 za kitanzania (50,000,000/=)
Katika Washindi 30 waliopatikana leo, washiriki wawili wameweza kuonyesha vipaji vyao huku washiriki hao wakiwa ni ndugu kabisa, washiriki hao ni babu na mjukuu wake wa kike ambao wameweza kufanikiwa kuingia hatua ya tatu kesho ambapo washindi wa Kanda ya Kati watapatikana.
Shindano la Tanzania Movie Talents linatarajiwa kumalizika kesho Kanda ya Kati Mkoani Dodoma na hatimaye kuhamia Kanda ya Juu Kusini ambapo usaili utafanyika Mkoani Mbeya na usaili wa Kanda ya Juu Kusini utaanza tarehe 19 April 2014 saa 1 asubuhi na wakazi wa Kanda ya Juu Kusini wanaombwa kujitokeza kwa wingi ili kuweza kuonyesha vipaji vyao na kuweza kuitumia fursa hii, Vilevile fomu za usaili zitapatikana Siku hiyohiyo ya usaili na fomu hizo hazina gharama yoyote ile.

No comments: