Advertisements

Wednesday, April 23, 2014

GUARDIOLA AZUNGUMZIA KUHAMIA KWAKE MAN UNITED, ASEMA...


KOCHA Pep Guardiola amekanusha tetesi za kuhamia Manchester United kutoka Bayern Munich anakopiga mzigo hivi sasa.
David Moyes amefukuzwa United na zikaibuka tetesi kwamba kocha huyo Mspanyola anapewa nafasi kubwa ya kurithi mikoba.
Lakini Guardiola ameruka kimanga mapema, akizungumza na Waandishi wa Habari katika mkutano maalum kuelekea mchezo wa Nusu Fainali ya kwanza Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Real Madrid.
Hakuna kitu kama hicho: Pep Guardiola amesema anabaki Bayern Munich na kukanusha tetesi za kuhamia Manchester Untied
Despair: David Moyes has been sacked by the club after less than a season in charge
Amepigwa chini: David Moyes amefukuzwa baada ya
karibu msimu mmoja wa kuwa kazini
Alipoulizwa kama ana nia ya kuhamia United, Pep alisema: "Nipo hapa. Nipo Bayern na ninataka kubaki kwa miaka miwili zaidi kumalizia kazi yangu. Tumeshinda taji la Bundesliga, lakini nafikiri timu inaweza kufanya vizuri zaidi. 
"Nafahamu vizuri kutoka staili ya ligi ya Hispania na kubadilisha kwenye staili ya Ujerumani haikuwa rahisi kwangu na ninahitaji muda zaidi ili kuhisi hii ni timu yangu haswa. 
"Nahisi kweli Bayern ni timu yangu, lakini nafikiri tunaweza kucheza vizuri na kuimarika. Kwa maana hiyo nafikiri nina kazi ya kufanya na ndiyo maana ninataka kubaki zaidi hapa. Niko vizuri hapana watu wanaamini kazi yangu,"amesema. Ryan Giggs ndiye kocha wa muda wa Man U kwa sasa.

No comments: