Advertisements

Wednesday, April 23, 2014

IBADA YA MSIBA WA MAREHEMU MARY MDEGELLA

Ndg zetu watanzania,
Fenista Msungu ( mtoto wa marehemu ) pamoja na wachungaji ( Malekela na Stella Swai ) tunatoa shukurani zetu kwenu nyote mliofika kutoa faraja na pole kwa mfiwa tarehe 22/4/2014 pamoja na kupiga simu, Mungu awabariki sana kwa moyo huo wa upendo na mshikamano.

Pia tunawapa taarifa kwamba ibada ya msiba tutaifanya tarehe May 3,2014 ambayo itakuwa siku ya Jumamosi saa 9 mchana hadi saa 12:30jioni (3pm-6:30pm). Anwani ya mahali pa ibada ni 12805 Georgia Avenue, Silver Spring MD 20906.

Mfiwa ataendelea kuwepo 3450 Tolledo Terrace #215, Hyattsville MD 20782 hadi tukapo wapa taarifa nyingine. Na mazishi yatafanyika kesho 24/4/2014 mjini Iringa, Tanzania yakiambatana na ibada fupi nyumbani kwa Mchungaji Malekela hapa USA mahali alipo mfiwa. Kwa maelezo piga simu240 604 2446 na 2404089446.

Imeletwa kwenu na uongozi wa Silver Spring Assemblies of God - ibada ya kiswahili.BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIBARIKIWE.

No comments: