Afisa kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Valerian Vitalis Kidole, akiendesha mafunzo ya siku nne ya wanahabari na watangazaji wa redio jamii yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO yaliyofanyika katika ukumbi wa Kartasi uliopo wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Na Mwandishi wetu
Wito huo umetolewa na Afisa kutoka Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika, Bw. Valerian Vitalis Kidole katika semina ya siku nne kwa waandishi wa habari na watangazaji wa redio jamii iliyomalizika mwishoni mwa katika ukumbi wa Kartasi wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.
Kidole alisema kuwa ili kuhakikisha jamii inapata lishe haina budi kutumia vyakula vile vinavyopatikana katika maeneo wanamoishi kuliko kusubiri vyakula vya msaada kutoka serikalini na vyakula kutoka viwandani.
Hayo yamezungumzwa katika mafunzo ya Kupunguza Madhara ya Maafa na kutoa Msaada wa Dharura yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO kwa ajili ya waandishi wa Habari na watangazaji wa redio jamii yanayofanyika Kahama wakati mwezeshaji akitoa mada ya Usalama wa Chakula nchini.
Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa chakula hutoa msaada wa chakula kwa wananchi pale kunapotokea upungufu wa chakula katika maeneo husika.
Aidha Kidole amesema kuwa chakula cha msaada kinachotolewa na serikali ni nafaka ambayo hayawezi kuboresha afya zao.
Katika halmashauri za mikoa nchini ambazo zina upungufu wa chakula, viongozi wa ngazi husika hawana budi kuwaelimisha wanachi juu ya kulima mazao mengi yanayohimili hali ya hewa husika na kwa wakati mwafaka ili kupunguza tatizo la upungufu wa chakula katika maeneo yao. Ni kwa namna hiyo jamii itaipunguzia serikali mzigo wa kutoa chakula cha msaada na badala yake kufanya shuguli nyingine za maendeleo.
Mkufunzi wa Redio Jamii kutoka UNESCO, Mama Rose Haji Mwalimu, akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari na watangazaji wa Redio jamii ya namna ya kuandaa jedwali maalum kwa ajili ya kuibua masuala katika utayarishaji wa vipindi kwenye mafunzo ya siku 4 yaliyomalizika mwishoni mwa juma mjini Kahama.
Msimamizi wa huduma za hali ya hewa kwa jamii kutoka Mamlaka ya hali ya hewa Tanzania (TMA), Hellen Msemo, akitoa mafunzo ya namna ya kuripoti taarifa sahihi za hali ya hewa kwa jamii kwa jamii na kuwaasa kuepuka upotoshaji wa taarifa za uongo kutoka kwenye vyombo visivyohusika zaidi ya mamlaka hiyo.
Baadhi ya waandishi na watangazaji wa redio za jamii nchini wakifuatilia kwa umakini mafunzo hayo yaliyofadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) kwa kushirikiana na UNESCO ambayo yamemalizika mwishoni mwa juma mjini Kahama.
Mwandishi wa Redio Jamii ya Pambazuko FM, Goodluck Msowoya, akielezea uzoefu wake kwa washiriki wenzake wakati wa mafunzo hayo ambapo amewataka kuwa na uthubutu kwa manufaa ya jamii.
Mwandishi wa Redio Jamii ya Pangani FM, Mwajabu Ali akiwasilisha kazi ya vikundi wakati wa mafunzo hayo yaliyomalizika mwishoni mwa juma mjini Kahama.
Mafunzo yakiendelea.
Washiriki wakiwa katika vikundi kazi.
No comments:
Post a Comment