Advertisements

Wednesday, April 16, 2014

KINANA AMALIZA ZIARA WILAYA YA MLELE KUHUTUBIA LEO MPANDA MJINI


 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana na ujumbe wake wakipata maelezo kutoka kwa Daktari wa Kituo cha Afya Inyonga Dk. Koni,Katibu Mkuu alitembelea kituo hicho ambacho kimeombewa kibali cha kuwa hospitali ya wilaya tangia mwaka jana mwezi februari lakini mpaka sasa maombi hayajajibiwa wala mkaguzi kutoka wizara ya afya hajafika kituoni hapo,kituo hicho ni kikubwa chenye vitanda 90 na uwezo wa kulaza wagonjwa 60 kwa mara moja,kina majengo ya kutosha na vifaa vya kutosha kuwa hospitali ya wilaya.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia baadhi ya vifaa vipya kabisa vya kituo hicho cha afya cha Inyonga wilayani Mlele ambacho kinaomba kupatiwa hadhi ya kuwa hospitali ya Wilaya .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akijaribu kuendesha Pikipiki ya kubebea wagonjwa iliyopo kwenye kituo cha afya cha Inyonga, kupewa hadhi kuwa hospitali ya wilaya hospitali hiyo itasaidia wananchi wengi wa wilaya ya Mlele kupata huduma karibu badala ya kusafiri umbali mrefu mpaka wilaya ya Mpanda,hasa kupunguza sana vifo vya Mama na Mtoto.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Inyonga wilaya ya Mlele mkoani Katavi na kuwapongeza kwa umahiri wao wa kuchapa kazi na kuchangia maendeleo yao na alisisitiza kuwa kero zinazowakabili za kupata hospitali ya wilaya, maji na umeme zitatuliwa mapema.

 Katibu Mkuu wa CCM akihutubia wananchi wa kata ya Inyimbo katika viwanja vya shule ya msingi Inyimbo
 Vijana wakiwa juu ya boda boda kuona mkutano vizuri mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alipohutubia kata ya Inyimbo wilaya ya Mlele.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akibeba tofali baada ya kulifyatua kwa kutumia mashine maalum ya kufyatulia matofali wakati wa kushiriki ujenzi wa ofisi ya CCM ,Inyimbo wilaya ya Mlele.
 Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Katavi Dk. Pudensiana Kikwembe akibeba tofali kusaidia ujenzi wa ofisi za CCM Inyimbo wilaya ya Mlele.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa maabara wa shule ya Sekondari ya Kata ya Mtapenda iliyopo kata ya Nsimbo wilaya ya Mlele.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akibeba tofali wakati wa kushiriki zoezi la kufyatua matofali ya kujenga tanki la maji katika mradi wa maji wa kijiji cha Mwenge wilaya ya Mlele mkoa wa Katavi utakaogharimu kiasi cha shilingi milioni 400.

No comments: