
Leo ni siku ya kumbukumbu ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Sheik Abeid Aman Karume miaka 42 iliyopita aliyeuwawa kwa kupigwa risasi huko visiwani Zanzibar. Sheik Abeid Karume na Mwalimu Julius Kambarage Nyerere waliandika historia ya nchi yetu na kutupatia Tanzania baada ya kuunganisha nchi zao yaani Tanganyika na Zanzibar na kuzaliwa Tanzania April 26, 1964 pamoja na kwamba kunamsuguano unaoendelea kuhusiana na muungano huu hususani Zanzibar. Bunge maalum la Katiba linaloendelea sasa hivi mjini Dodoma Muungano ni moja ya mambo yatayozungumuziwa.
Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani utasherehekea miaka 50 ya Muungano kitaiafa hapa Washington, DC kwa sherehe hizo kuanza saa 3 asubuhi (9am) siku ya Jumamosi April 26, 2014
No comments:
Post a Comment