Mbunge wa Ubunge,John Mnyika
Mbunge wa Ubunge, John Mnyika, amemtaka Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik, kutoa ufafanuzi kwa umma sheria aliyoitumia kuzuia pikipiki na bajaj kuingia katikati ya Jiji.
Kauli ya Mnyika inafuatia Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam, kunukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari akisema kwamba hawezi kusitisha kwa muda agizo lake la kukataza pikipiki na bajaj kuingia katikati ya Jiji.
Sadik pia alinukuliwa kuwa hawezi kufanya hivyo kwa kuwa agizo hilo si lake bali la sheria ambayo ameamua kuisimamia.
Alitoa kauli hiyo kufuatia taarifa ya Mnyika ya Aprili 2, mwaka huu aliyomwandikia ujumbe kutaka asitishe kwa muda utekelezaji wa tamko alilotoa Machi 3, mwaka huu ili kupisha mazungumzo baina ya serikali, wahusika wa bodaboda, bajaj na wadau wengine muhimu ili kupata ufumbuzi.
"Kufuatia kauli hiyo ya Mkuu wa Mkoa, nimeipitia kwa mara nyingine tena kifungu kwa kifungu sheria inayohusika ambayo ni The Surface and Marine Transport Regulatory Authority Act; Sheria namba 9 ya mwaka 2001.
Hakuna kifungu chochote katika sheria hiyo kinachokataza pikipiki/bodaboda au bajaj kuingia katika maeneo ya katikakati ya jiji," alisema Mnyika katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana.
Aliongeza: "Mkuu wa Mkoa anapaswa kuzingatia kwamba eneo linaloitwa katikati ya Jiji ambalo pikipiki/bodaboda na bajaj zimepigwa marufuku mipaka yake kwa barabara ya Morogoro ni Ubungo, barabara ya Uhuru ni Buguruni, Barabara ya Nyerere ni Tazara na Barabara ya Kilwa ni Chuo cha Uhasibu; na hivyo kuleta mgogoro na kuwakosesha wananchi huduma."
Alisema Mkuu wa Mkoa anapaswa kuzingatia kwamba sheria hiyo kifungu cha 5, kimetamka kwamba wajibu wa Sumatra, ni pamoja na kulinda maslahi ya watumiaji wa huduma na kuhamasisha upatikanaji wa huduma ikiwamo kwa wateja wa kipato cha chini.
"Usafiri wa pikipiki/bodaboda na bajaj siyo tu umetoa fursa ya ajira kwa vijana, bali pia unasaidia wananchi wa kipato cha chini na unasaidia mazingira ya foleni katika Jiji la Dar es Salaam.
Hivyo, agizo la kutaka usafiri huo uishie Buguruni, Ubungo, Tazara na Chuo cha Uhasibu, ni suala ambalo limeibua mgogoro unaostahili ufumbuzi wa haraka," alisema.

SOURCE: NIPASHE
No comments:
Post a Comment