ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 6, 2014

MATOKEO YA AWALI YA UCHAGUZI WA MBUNGE KATIKA JIMBO LA CHALINZE

Matokeo ya awali
Kata ya Pera; Malivundo Ofisi ya Mtendaji; CCM 77, CHADEMA 2, CUF , AFP 1, NRA 1.
Kimbugi; CCM 11, CHADEMA 1, CUF 0, AFP 0, NRA 0
Magange Ofisi ya Kitongoji; CCM 101, CHADEMA 1, NRA 0, AFP 0
Pingo Shule ya Msingi Namba 1; CCM 31, CHADEMA 1, CUF 1, NRA 0, AFP 0 
Pingo Ofisi ya Kitongoji Namba 2; CCM 61, CHADEMA 4, CUF 2, AFP 1, NRA 0
Pingo Namba 1; CCM 66, CHADEMA 0, NRA 0, AFP 0

- Matokeo ya awali kwa baadhi ya vituo yanaonesha kuwa mgombea wa CCM Ridhiwani Kikwete anaongoza kwa kiasi kikubwa.
- Kazi ya kuhesabu kura katika Jimbo la Chalinze imeanza na matokeo yatatangazwa muda wowote kuanzia sasa.

- Baadhi ya wagombea wa vyama vya upinzani ikiwa ni pamoja na CHADEMA wamelalamikia mwenendo wa uchaguzi wa ubunge Jimboni Chalinze.

- Rais Kikwete na mkewe mama Salma Kikwete wamejitokeza kupiga kura katika kituo cha shule ya Msingi Msoga kuchagua mbunge wa Chalinze.
- Wakazi wa jimbo la Chalinze wamejitokea kwa wingi kupiga kura kumchagua mbunge wao. Zoezi limemalizika kwa amani na utulivu.

 Wakati huo Kurugenzi ya Habari CHADEMA imeelezea HALI ILIVYOKUWA NA MATOKEO YA AWALI CHALINZE kama ifuatavyo:-

Uchaguzi wa mdogo wa Jimbo la Chalinze umefanyika huku ukigubikwa na kasoro kadhaa, ikiwa ni pamoja na watu wachache kujitokeza vituoni kupiga kura, wapiga kura kulalamika ‘kupokwa’ vitambulisho vyao, vituo kuwa majumbani kwa watu, huku pia kukiwa na hofu ya vurugu.

Kasoro hizo zilijidhihirisha jana wakati wapiga kura shughuli ya upigaji kura ilipokuwa ikiendelea katika maeneo mbalimbali ya jimbo hilo ambapo wananchi wa Chalinze walikuwa wakipiga kura mbunge wao, kuziba nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Said Bwanamdogo aliyefariki mapema mwaka huu.

1 comment:

Anonymous said...

ukweli utabaki palepale Rithiwani ataongoza tu kule kwao baba yake raisi wa Tanzania unategemea watampa mtu baki wakati mzawa yupo?yani hapo kama vile umpeleke Rithiwani akagombee ubunge Mwanga Kilimanjaro hawatampa watamtaka Msuya au Maghembe aliyerithishwa na Msuya,Hongereni chalinze kwa kumpa mwana wa hano kura.Poleni chadema hakuna uchaguzi unaopita kwenu kimya bila kulala mika.