Katika hali ambayo maelezo yake ni kwamba CCM wamekuwa hawana uhakika wa kushinda ubunge Jimbo la Chalinze, huku wakiwa na hofu ya kushindwa, gari lao moja aina ya Land Cruiser, T630 BFJ, limekutwa na silaha mbalimbali, kama vile mikuki, mapanga, sime na marungu, huku likimwinda kwa kumfuata kila anakokwenda mgombea ubunge wa CHADEMA, Mathayo Torongey, wakitaka kumdhuru.
Gari hilo lilikuwa likiongozwa na Katibu wa CCM, Wilaya ya Mfindi, Issa Mtaturu ambaye alionesha jeuri ya ajabu akiwa mbele ya askari polisi waliokamata gari ile baada ya Torongey kutoa taarifa kwa polisi waliokuwa karibu.
Kitu cha kushangaza ni kwamba gari hiyo ilipewa maelekezo iende yenyewe au watuhumiwa hao wajipeleke Kituo cha Polisi Chalinze, kisha polisi watawakuta hapo. Kiongozi yule wa CCM akajibu kwa jeuri kuwa watakwenda wakishamaliza kazi zao. RPC ameshindwa kuchukua hatua zozote za maana juu ya tukio hilo.
No comments:
Post a Comment