ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 30, 2014

Mpoki Safarini Dar/UTU yapata Viongozi Wapya

 Mchekeshaji maarufu   kutoka nchini Tanzania  Muarabu wa Dubai a.ka Mpoki ameondoka nchini Ujerumani kurudi nyumbani Tanzania baada ya ziara yake ya siku 4 kukamilika. Msanii huyo ambaye alifanya ziara nchini ujerumani baada ya kualikwa na Umoja wa wa Watanzania  Ujerumani (U T U) kwa ajili ya Sherehe za muungano wa Tanzania, zilizoambatana na kongamano la kibiashara pamoja na  Mkutano mkuu  wa uchaguzi wa        U T U.
Mchekeshaji huyo maarufu kutoka kundi la Orijino Komedi  aliweza kuburudisha waliohudhuria katika sherehe hizo kubwa na za aina yake katika jiji La Berlin Ujerumani.
 Kufuatia uchaguzi mkuu wa U T U.  Bw. Mfundo Peter Mfundo amepata ushindi  mkubwa wa % 98 na kuendelea kuwa Mwenyekiti wa U T U kwa kipindi kingine cha miaka 2.
 Nafasi ya makamo Mwenyekiti  ilinyakuliwa na Bw. Peter Kazaura nafasi ya Katibu imechukuliwa na Bi. LiLian Sorogo, nafasi ya  Muweka hazina  imechukuliwa na  Rajab Kaoneka.
 Wajumbe wa kamati ni. Zenat Jamal, Dr. Andreas Wesselmann, Julius Tsaxarra, Joyce Rupia, Vital kazimoto, na Fulgens Kisalya. Mutano huu wa Uchaguzi ulihudhuriwa na Mgeni Rasmi Mh. Naibu Balozi wa Tanzania nchini ujerumani Bw. Mvulla.
Mwenyekiti wa U T U  Bw Mfundo Peter amesema timu yake mpya inategemea kubadilisha sura nzima na mwenendo wa Umoja  huu, ndani ya kipindi cha miezi 6 ya uongozi mpya. Chanzo cha habari kilinyetisha
Baada ya  mkutano  wa uchaguzi kumalizika mnamo saa 11:30 alasiri, Viongozi wa U T U na Wanachama  walijumuika na watanzania wengine katika tafrija ya chakula cha jioni katika Hotel ya MARITIM HOTEL Berlin.  ambayo iliandaliwa rasmi na Ubalozi wa Tanzania nchini ujerumani ili kuhitimisha sherehe za Muungano wa Tanzania katika Tafrija  hiyo kubwa  walihudhuria wageni mbali mbali, Diplomats, na burudani mbali mbali zilikuwepo zikiwemo ngoma  za asili kutoka Tanzania na Vichekesho kutoka kwa Mchekeshaji  MPOKI, pia kulikuwa na Muziki wa kunesanesa. Msanii wa Movie na mtayarishaji wa kipindi cha Beyond the Borders bi Devota Alfred aliweza kufanya mahojiano na wasanii pamoja na viongozi waliohudhuria sherehe hizi. naye mtangazaji wa Deutsche welle idhaa ya kiswahili Bw Sudi Mnete hakuwa mbali siku hii akirepoti kutoka katika eneo la tukio.

No comments: