Balozi Ramadhan Mwinyi, Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, akizungumza katika Chemba ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa wakati wa mkutano wa siku moja wa Baraza hilo uliofanyika juzi ( jumatatu) mkutano huo ulihusu mageuzi ya sekta za usalama, ambapo kwa mara ya kwanza Baraza Kuu la Usalama lilipitisha Azimio linalojitegemea kuhusu mageuzi katika sekta za usalama. Tanzania ilikuwa miongoni mwa nchi 42 zilizochangia majadiliano hayo yaliyofunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon ambapo hoja iliyozungumzwa na wengi ni umuhimu wa nchi kumiliki mchakato wa mageuzi ya sekta za usalama. Nyuma ya Balozi, ni Lt. Kanali Wilbert Ibuge, Mwambata Jeshi katika Uwakilishi wa Kudumu
Na Mwandishi Maalum
Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, imeungana na mataifa
mengine katika kusisitiza umuhimu wa nchi kumiliki mchakato wa Mageuzi ya Sekta za Usalama ( Security Sector
Reform)
Akichangia majadiliano
ya Baraza Kuu la Usalama la Umoja wa Mataifa ambalo lilikutaka kwa siku nzima ya jumatatu kujadili taarifa
ya Katibu Mkuu kuhusu SSR. Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katikak UN,
Balozi Ramadhan Mwinyi amesema, Tanzania
kama ilivyo kwa nchi nyingine nyingi
inapenda kuona kwamba mageuzi ya
sekta za usalama yanamilikiwa nan chi zenyewe
zikiwamo nchi zinazotoka katika
machafuko.
Katika Mkutano huo wa jumatatu, Baraza Kuu
la Usalama la Umoja wa Mataifa, lilipitisha kwa kauli moja na kwa mara ya kwanza Azimio
linalojitegemea kuhusu mchakato wa
Mageuzi ya Sekta za Usalama.
Kupitia azimio hilo namba
2151 (2014) pamoja na kusisitiza umuhimu
wa dhana zima ya mageuzi ya sekta za usalama na
umuhimu wake kwa usalama, amani na ustawi wa mwanadamu. Azimio
linasisitiza kwamba umiliki wa nchi
katika mageuzi hayo ni jambo la muhimu
Akaongeza kuwa makundi ya
wapiganaji na ambao wameka silaha zao chini na
kuingia katika mchakato wa majadiliano wanapashwa pia kuwa sehemu ya
mageuzi ya sekta za usalama.
Akasema kwa kuyashirikisha
makundi hayo ya wapiganaji na mengine
kutasaidia ujenzi wa Amani na
usalama na pia kuepusha kujirudia kwa mapigano.
Aidha Balozi Mwinyi, ameleza kwamba, nchi zinazopakana
na nchi zinazotoka kwenye machafuko pia
zinayonafasi na wajibu wakutoa
ushirikiano na uzoefu wao katika ujenzi wa sekta za usalama.
Vile vile Balozi
amebainisha kwamba katika miongo ya
miaka mitano iliyopita imedhihirisha
wazi umuhimu wa jumuia za kikanda
katika uzuiaji wa mapigano, ulinzi wa
Amani na ujenzi wa Amani.
Majadiliano hayo
yalifunguliwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na yaliitishwa na Nigeria ambayo ni Rais
wa Baraza hilo kwa Mwezi huu wa April.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Nigeria Bw. Aminu Wali aliongoza majadiliano.
Wawakilishi kutoka nchi 42 wanachama wa Umoja wa Mataifa,
zilizungumza wakati wa majadiliano kuhusu dhana hiyo ya mageuzi ya sekta za usalama, na
bila ya kujali tofauti zao, kila moja
ilisisitiza hoja ya nchi kumiliki mchakato huo hata kwa zile ambazo zimetoka katika machafuko au
mapigano.
Aidha pamoja na kusisitiza
haja na umuhimu wa nchi kumiliki mchakato huo, zimeongeza kuwa bado kuna haja
ya Jumuiya ya Kimataifa, kuziwezesha nchi hasa zile zinazotoka katika
machafuko kuweza si kujenga upya sekta hizo za usalama bali pia kuzifanyia
mageuzi.
Vile vile ilielezwa
ilisisitizwa pia kuwa mageuzi hayo ya
sekta za usalama ni muhumu katika
kuziimarisha nchi ambazo ndiyo kwanza zimetoka kwenye machafuko. Na
kwamba mageuzi hayo yatapewa kipaumbele
katika utekelezaji mamlaka za
ulinzi wa Amani na misheni za
maalum za Kisiasa
Wajumbe wengine walikwenda
mbali zaidi, kwa kueleza kwamba mageuzi hayo ya
sektza za usalama yanapashwa kuwa jumuishi kwa maana ya kushirikisha makundi mengine ya kijamii.
Lakini kwa msisitizo kwamba serikali ndiyo iwe na mamlaka ya kuamua mfumo wa
sekta zake za usalama.
Katika salamu zake za
ufunguzi Ban ki Moon, alisema, lengo la kutekeleza mageuzi ya sekta za
usalama ambazo ni pamoja na jeshi, polisi na vyombo ya usalama ni
kuwawezesha wananchi ambao ndiyo walengwa kuisha maisha yenye
usalama.
“Sekta za Usalama ndiyo muhimili mkuu wa makubaliano kati ya serikali na wananchi wake. Mamlaka ya kutumia nguvu ni lazima yaendane na wajibu wa kulinda raia na kuheshimu haki za binadamu” akasema Katibu Mkuu.
Kwa mujibu wa Ban Ki Moon, sekta za usalama zinazotekeleza majukumu yake chini ya misigi ya utawala wa sheria
zinauwezo wa kuimarisha imani ya wananchi kwa serikali yao na hivyo kuchangia
katika uimara wa ujenzi wa Amani na maendeleo.
No comments:
Post a Comment