Mto
Ruaha ni moja ya mito ambayo maji yake kwa kiasi kikubwa sio masafi
yamechanganyikana na tope, hali hiyo imesababisha kuwa na mazalio mengi
ya samaki aina ya Kambale, Samaki hao ambao wanauwezo wa kuishi kwa
muda mrefu hata kama hakuna maji kutokana na kwamba huwa na uwezo wa
kujizika ndani ya tope hata kwa miezi zaidi ya sita.
Wavuvi
wa eneo hilo wamekuwa wakijishughulisha na uvuvi wa samaki aina
mbalimbali lakini zaidi huvua samaki aina ya Kambale, Hivi karibuni
wamevua Kambale mkubwa sana na kukili kwamba alikuwa ni moja ya samaki
wakubwa ambaye wamemvua.
Wamesema kwamba walisha wahi kuvua samaki aina hiyo mkubwa lakini hakufikia samaki huyo aliyevuliwa hivi karibuni.
"Ni kweli tumekuwa tukivua sana samaki lakini huyu ni samaki mkubwa sana ambaye tumemvu" aliongea Mvuvi.
Huyu ni Samaki Mkubwa ambaye alionekana pembezoni mwa Mto Ruaha Iringa Mara baada ya Kuvuliwa tayari kwa kuingizwa Sokoni.
Samaki huyo akiwa anaonekana kwa ubavuni.
Picha na Iringa yetu
No comments:
Post a Comment