Kamishna wa Chama cha Mpira wa Kikapu Marekani (NBA) amemfungia
maisha bwana Donald Sterling kujihusisha na Clippers au NBA, adhabu hiyo
ilitangazwa siku ya
Jumanne kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Manhattan.
Bwana Silver pia amempiga faini bwana Sterling ya dola milioni 2.5, kiwango cha juu kabisa kinachoruhusiwa na Katiba ya NBA.
Pesa hizo za faini zitatolewa kama msaada kwenye mashirika yanayopingana na ubaguzi na juhudi za uvumilivu ambazo zitaungana na kuchaguliwa na NBA na
Chama cha Wachezaji. Ikiwa ni adhabu ya maisha, Sterling hatohudhuria mechi au mazoezi ya NBA, kuwepo kwenye ofisi au miradi ya Clippers au kushiriki kwenye biashara au maamuzi ya mchezaji yanayohusiana na timu.
Pia hatoruhusiwa kuhudhuria kwenye vikao vya Bodi ya Magavana na kushiriki kwenye shughuli zozote za ligi.
Kamishna Silver pia alitangaza kwamba ataihimiza Bodi ya Magavana kutekeleza uongozi wake kulazimisha kuuzwa kwa timu.
Adhabu hiyo ilitolewa siku ya Jumanne kutokana na maamuzi ya Kamishna huyo kwamba Sterling alikiuka sheria za ligi kwa kutoa kauli chafu na za kuumiza, na athari yake kuonekana kwa kiasi kikubwa kwenye ligi nzima.
Karatasi ya taarifa hiyo ambayo Kamishna Silver aliitumia wakati wa mkutano na waandishi wa habari itatolewa leo mchana na kutumwa kwenye mtandao wa NBA.

No comments:
Post a Comment