Kesi ya kutakatisha fedha haramu inayomkabili wakili maarufu jijini hapa, Median Mwale na wenzake watatu akiwamo Meneja wa Benki, imechukua sura mpya baada ya upande wa utetezi kudai kesi hiyo ilifunguliwa kimakosa kabla ya sheria iliyowashtaki kutungwa.
Kwa msingi huo, washtakiwa wameomba kesi hiyo kuhamishiwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kupata tafsiri ya kisheria.
Aidha, wamelalamikia ucheleweshwaji wa makusudi wa kuanza kusikilizwa kwa shauri hilo waliodai unafanywa na upande wa serikali kwa kigezo cha upelelezi kutokamilika huku wateja wao wakiendelea kusota rumande kwa miaka mitatu sasa.
Madai hayo yalitolewa na Wakili wa utetezi, Omary Iddi Omary, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Devota Kamuzora.
Wakili Omary anasaidiana na mawakili Moses Mahuna na Modest Akida, huku upande wa Serikali ukiwakilishwa na Wakili Tumaini Kweka.
Mbali na Wakili Mwale, washtakiwa wengine ni Elius Ndenjembi, Don Bosco Gichana na Boniface Mimbwa.
Moyo ambaye aliwasilisha hoja nne tofauti akitaka mahakama hiyo iwape idhini ya kwenda Mahakama Kuu, alidai kuwa hata shitaka lingine walilofunguliwa wateja wake chini ya Sheria ya Uzuiaji utakasaji fedha haramu ya mwaka 2006, ina mapungufu makubwa kisheria inayoifanya isiwe halali kisheria.
Alidai kuwa sheria hiyo iliwekwa kwenye Gazeti la Serikali Januari 12, mwaka 2006 kabla ya kusainiwa na Rais Januari, 2007, jambo alilodai kuwa linakwenda kinyume na Katiba ya nchi.
“Mheshimiwa hakimu, kutokana na ukiukwaji wa taratibu hizo, inafanya Sheria ya Uzuiaji Utakasaji Fedha Haramu ya mwaka 2006 isiwapo.
Hii ina maana hata washtakiwa hawa wanashikiliwa kwa kutumia sheria ambayo haipo, hata kosa wanaloshtakiwa nalo halipo kwenye sheria za sasa. Katika mazingira hayo, hakuna shaka kuwa hapa hakuna mashitaka sahihi,” alidai Wakili Omary.
Kwa upande wake, Wakili wa Serikali, Kweka akijibu hoja hizo alidai kuwa hazina msingi kwa madai kuwa sheria hutumika baada ya kupitishwa na Bunge na kuwa imefuata michakato yote ndipo ikaanza kutumika.
“Nafikiri wameleta malalamiko kwenye eneo lisilo sahihi, kwani hata kwa mujibu wa uanzishwaji wa mahakama, hii sidhani kama wewe (hakimu), unaweza kuamua mashauri ya Manyara.
Hii ni sawa na kumtuma mtoto akachukue chakula cha mlinzi,” alisema Wakili Kweka, jambo lilomfanya hakimu kuingilia kati na kumtaka afute kauli yake hiyo ya kumfananisha yeye na mlinzi.
Hata hivyo, wakili huyo alisisitiza kuwa shauri hilo lipo mahakamani hapo kwa ajili ya kuahirishwa na kupangiwa tarehe nyingine kwa maelezo kuwa mahakama hiyo haina nguvu kisheria kulisikiliza.
Akijibu hoja hiyo wakili wa washtakiwa, Omary alisema kuwa hata wao wanajua kuwa mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza shauri hilo ndiyo maana wanaomba kupewa idhini kwenda Mahakama Kuu wakapatiwe ufafanuzi wa kisheria juu ya yale wanayoyalalamikia.

CHANZO: NIPASHE
No comments:
Post a Comment