ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, April 16, 2014

[New Video] Nameless “Ng’anga’ana”



url
Mwanzoni mwa mwaka huu kulitokea uvumi kuwa msanii Nameless kutoka nchini Kenya atastaafu shuguli za muziki mwaka huu, yaani 2014, Uvumi huo ulitokana na jina la album mpya ya Nameless ambayo inatarajiwa kutoka mwaka huu. Album iyo itakua ikiitwa ‘B4IR’ (Before I Retire) tafsiri yake kwa kiswahili ikiwa ni ‘Kabla Sijastaafu’.
Baada ya kuenea kwa
uvumi huo Nameless ambae ni msanii mkongwe sana anaejulikana sana nchini kenya na Mashariki mwa Afrika kwa ujumla, aliamua kujitokeza na kutolea ufafanuzi kuhusu jina la album hiyo na  alisema kuwa album hiyo itaelezea mambo mengi atayofanya kabla ya kuacha muziki, akaongezea kuwa hajafikiria kustaafu siku za karibuni. Wiki iliyoisha Nameless alitambulisha wimbo wake mpya unaoitwa ‘African Beauty’ ambao ndio wimbo wa kwanza kutoka katika album yake hiyo mpya.
Zikiwa zimepita siku chache tu tangu aachie ‘African Beauty’, Nameless kaamua kuachia video ya nyimbo yake ya pili ambayo nayo inapatikana kwenye Album hiyo. Video hiyo yenye mahadhi ya reggae aliyoipatia jina “Ng’anga’ana” na inaelezea maisha ya kila siku wanayokutana nayo wananchi wa Kenya.
Unaweza itazama video hiyo hapa chini

No comments: