Advertisements

Wednesday, April 16, 2014

KURA KUHUSU AINA YA MUUNGANO KUPIGWA AGOSTI

Upigaji kura kupitisha sura mbili zinazohusu Muungano katika Bunge la Katiba umesogezwa mbele hadi Agosti litakapoitishwa tena, Mwananchi limebaini.
Upigaji kura hautafanyika sasa badala yake wajumbe wa
Bunge wataendelea kuchangia hoja hadi Aprili 28, mwaka huu wakati Bunge hilo litakapoahirishwa baada ya kukamilisha siku 70 za awali.
Awali, upigaji huo wa kura ambao umewagawa wajumbe katika makundi mawili; moja likitaka serikali tatu na jingine likitaka serikali mbili, ulitarajiwa kufanyika Ijumaa wiki hii ili kuhitimisha mvutano wa muda mrefu baina ya pande zinazopingana.
Mwenyekiti wa Bunge, Samuel Sitta alithibitisha kuahirishwa kwa upigaji wa kura huo, lakini akasema hiyo imetokana na wingi wa wajumbe wanaotaka kuchangia na si kitu kingine. Hivyo Bunge hilo linatarajiwa kuanza tena shughuli zake tarehe 5 Agosti.
“Ni kweli wajumbe hawatapiga kura kwa sura mbili walizowasilisha hadi jana na lengo ni kuwapa nafasi wajumbe wengi zaidi kuchangia katika jambo hili zito,” alisema Sitta.
Alisema hadi jana mchana alikuwa amepokea majina ya wachangiaji zaidi ya 400 ambao wasingeweza kuchangia kwa siku tatu kama kanuni zinavyoelekeza.

No comments: