ANGALIA LIVE NEWS

Monday, April 7, 2014

NINI HATMA YA WATOTO HAWA WAKIRUDI TANZANIA BAADA YA USHINDI HUU ULIOITANGAZA NCHI YETU CHAMA CHA SOKA TFF NA SERIKALI

WATOTO HAO BAADA YA KUSHINDA WAKIWA NA BOSI WAO MUTANI YANGWE..


Hatimaye Tanzania imegusa anga za mafanikio kidogo, baada ya kuondoka kwa siku chache kwenye anga za kichwa cha mwendawazimu kwa timu yake kutwaa ubingwa wa juu kabisa wa soka.
Timu ya Taifa ya Watoto wa Mitaani ya Tanzania imetwaa ubingwa wa Dunia wa Watoto wa Mitaani baada ya jana (Aprili 6 mwaka huu) kuilaza Burundi mabao 3-1 katika mchezo wa fainali uliochezwa jijini Rio de Janeiro, Brazil.
Mshambuliaji Frank William alifunga mabao matatu katika mechi hiyo iliyochezwa uwanja mkongwe na maarufu wa klabu ya Fluminense huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Fedha wa Uingereza, George Osborne.
Tanzania ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuitandika Marekani mabao 6-1 ambapo hadi mapumziko ilikuwa mbele kwa mabao 4-0.
Burundi ilipata tiketi ya kucheza fainali baada ya kuifunga Pakistan mabao 4-3 katika mechi ya nusu fainali ya pili.
Timu ya Tanzania inarejea nchini Alhamisi (Aprili 10 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 10 jioni kwa ndege ya Emirates.
CREDIT:SALEHJEMBE

3 comments:

Anonymous said...

Kwa uzoefu tulionao, vijana hawa ambao kwakweli wamefanya kazi nzuri sana, watapokelewa kwa vifijo, probably wanaweza kualikwa kwa mkuu kula ubwabwa then ndio utakuwa mwisho wao.kila mmoja wao atajiendeleza kwa jitihada zake.

Anonymous said...

Mdau hapa juu ninaungana nawewe kabisa, yetu macho ndugu zanguni hawa watoto na wanaowaongoza wamefanya kazi nzuri sana ambayo Taifa na TFA pamaoja na wapenda mizhezo wote na matajiri wote. Ushabiki wa kuzogodea fedha kwenye clabu za SIMBA na YANGA nafikiri ni nyingi zaidi ya hizi ambazoi zingeliweza kuwaweka hawa vijana kambini na wakafanya vizuri hata kuzifunga YANGA au SIMBA. Tunaomba chonde chonde waache kudanganywa toto na wapatiwe huduma na malezi ya kujenga mpira wa kizazi kijacho na sio SIMBA NA YANGA TU. Tusishangae wakapokelewa kwa ubwabwa na ikawa ndio lala salama jamani VIONGOOOOZI WA SOKA LA TANZANIA JAMANI KUWENI NA HURUMA NA MSIWANYANYASE VIONGOZI WA HII TIMU. Tatizo la viongozi wanapenda sana fedha kuingia mikononi mwao na kuwaburuza waandaaji.

Anonymous said...

bado kama niko ndotoni kwani timu hii ilipatikana vipi?