Advertisements

Friday, April 18, 2014

Prof.Baregu aitahadharisha CCM mchakato wa Katiba

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba,Profesa Mwesiga Baregu.

Mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Profesa Mwesiga Baregu, (pichani) amekitahadharisha Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuachana na msimamo wake katika mchakato mzima wa kupata Katiba mpya.

Profesa Baregu amesema hatua hiyo ya CCM mwishowe itawagharimu kwa kuliingiza taifa kwenye mtafaruku mkubwa utakaosababisha uvunjifu wa amani.

Amesema misimano isiyo na tija na mbinu chafu ambazo CCM wanajaribu kuzifanya ili kupenyeza mipango yao ambayo haikubaliki kwa wananchi, ni hatari na inaweza kusababibisha machafuko makubwa nchini.

Profesa Baregu, aliyasema hayo katika mahojiano maluum na NIPASHE na kueleza kuwa vitendo vinavyojitokeza katika Bunge hilo Maalum la Katiba, ni wazi kwamba kuna watu wameingia kwenye Bunge hilo bila kuelewa lengo lake.

Profesa Baregu alisema kuwa Bunge hilo siyo kwa ajili ya kupigana vikumbo, isipokuwa ni kwa ajili ya kutengeneza mfumo ambao utaleta maelewamo kwa ajili ya mustakabali wa nchi na wananchi wake.

"Hivyo kutokana hali ilivyo, ni wazi kuwa Chama tawala ndiyo kinaweka misimamo yake juu ya maslahi ya taifa, suala hilo halitakubalika na badala yake kuna hatari ya kuleta machafuko," alisema Profesa Baregu.

Aliongeza: "Kwa mantiki hiyo, Watanzania wanaotegemea Katiba inayotokana na mchakato wa maoni yao kwa maslahi ya nchi, wasipoipata na wakaletewa Katiba iliyobeba matakwa ya CCM, kuna uwezekano mkubwa wa kuleta mtafaruku mkubwa kama ilivyotokea nchi jirani ya Kenya," alisema Profesa Baregu.

Aidha, alisema kama Katiba haitapatikana na kuingia kwenye uchaguzi bila Katiba mpya, uchaguzi huo hautakuwa huru.

"Wanaofanya mchezo na Katiba wasidhani kuwa watapata Katiba ya sehemu fulani ama ushindi wa kitu fulani, lakini wafahamu kuwa zao la Katiba ni la zao la kile walichochangia wananchi wenyewe," alisema.
CHANZO: NIPASHE

2 comments:

Anonymous said...

Absolutely Right. Mheshimiwa Prof. Baregu unaona mbali. Hii ni wazi CCM haiitakii Tanzania amani tena. Fedha wameshakula nyingi tu huu mchakato bora usitishwe. Angalia hata daftari ka wapiga kura limejaa waliokufa tayari na CCM bado inawaorodhesha. Bila kuangalia daftari hilo basii uchaguzi ujao ni feki na hali itakuwa tete. Mhe Sita anaburuza sana bunge hili.

Anonymous said...

Waambie hao wajinga wasiokuwa na hoja.ukawa wamekwenda kujinufaisha matumbo.na si kitu walichotumwa na wananchi.kuwa kama msomi usiwe kama wale wale wanaokataa ukweli na kukimbia Basra ya kulipwa pesa za walipa kodi.na washauri Chaka chako kikampime aioli huyo tundu Liau.pamoja na lipumba kwanza.