ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 15, 2014

SENTENSI 8 ZA ALICHOSEMA BUNGENI MH. JANUARY MAKAMBA

Mh. January Makamba.

Bunge la katiba linaendelea hapa Dodoma ambapo wajumbe wake mbalimbali wameindeleza ishu ya uwepo wa Serikali tatu na wengine serikali mbili ambapo yafuatayo kwenye post hii ni aliyoyasema Mh. January Makamba.

1. ‘Kama tunataka kuuvunja muungano wetu ndani ya mwaka mmoja au miwili…. tuingie kwenye serikali tatu, itakua ni janga kubwa sana kuiua hii lulu’

2. ‘Nchi nyingi za Afrika zimetengenezwa na mipaka ya Wakoloni, sisi Waafrika ndio tumetengeneza kitu chetu wenyewe na tukakipa jina wenyewe na kukiita Tanzania, kama tunataka ulimwengu utucheke… tuue kitu chetu wenyewe’

3. ‘Nimeisoma rasimu, ukitazama kitu cha kwanza baada ya sisi kupitisha serikali tatu tunakwenda kwenye mpito ambako kwenye masharti ya mpito ibara ya 269 kifungu cha kwanza kinaeleza mambo yatakayofanyika kwenye kipindi cha mpito, ni kugawana mali, madeni na watumishi’

4. ‘Kitendo cha kugawana mali, kugawana madeni, kugawana Watumishi…. kitendo cha kugawana hivyo vyote ni kitendo cha utengano’

5. ‘Kwenye mgawanyo huohuo wa kugawana mali hata kabla hatujaanza kwenye serikali hii ya shirikisho ndio itakua mwisho hapohapo, tukipitisha hii kitu.. mwaka mzima miaka miwili tutahangaika na mjadala wa kugawana’

6.‘Sisi wengine tumo humu baadhi yetu tutakuja kuongoza nchi hii, hatutaki kuja kuongoza taifa ambalo tunahangaika na taratibu za kugawana mali, taratibu za utengano’

7. ‘Viongozi tunaokuja tunataka kulijenga taifa kubwa na lenye nguvu zaidi na tutalijenga kama tutakua na umoja, hatutapenda kuhudhuria vikao vya kugawana mali, tunazo kazi nyingi za kimaendeleo… watu wetu wana mahitaji mengi’

8. ‘Tumetumia muda mrefu sana hapa kubishana kuhusu takwimu, ziko namna mbili za kujua utashi wa watu kwenye mambo makubwa, ya kwanza ni kupiga kura ya maoni kuwauliza wanataka nini… hatujalifanya bado, la pili ni kutazama matokeo ya uchaguzi na sera za vyama kuangalia chama gani kimeshinda hivyo kujua ni sera gani inayotakiwa’-GPL

2 comments:

Anonymous said...

Its about time MTU kasema ukweli hapo mstari wa 8. Either muungano uvunjike au tuwe name serikali moja since we are united. Muda umefika wa kufanya cha ukweli....let people vote maana bungeni hamna kitakacho fanyika zaidi yakuwalipa pesa wanaoingia bungeni

Anonymous said...

January asante ila tuliza boli na acha kujipigia debevkiaina. Bado waati wako haujafikia hatuwezi kuongozwa na aina uitakayo. Kaa hapo ulipo si ajabu hata miaka kumi uendelee na azi zabubunge Bumbuli kwani bado wako nyima saa...