ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, April 15, 2014

SHOGA! KITOE CHUMA KUTU UPATE RAHA KILA KONA


Jamani wee, kila nikitaka kukaa kimya mdomo unanicheza, siwezi kukaa kimya moja kwa moja lazima nitie neno ili kuhakikisha mambo yanakwenda sawa. Leo wari wangu nataka ni niwape somo la bure kuhusu kulinda nyumba zetu.

Tumekuwa tukilalamika tu kuwa waume zetu hawaoneshi kufurahia mapenzi tukiwa faragha. Wiki mbili nilielezea kupewa uhuru, sasa umeupata ufanyie kazi. Inawezekana uliyenaye ni mgeni wa mambo ya chumbani, nawe kama siyo mbunifu wa kujua uliyenaye ni ‘maimuna wa mapenzi’ basi penzi lenu linakuwa bora liende.

Waweza usione hasara zake mapema, lakini hasara zake huwa kubwa ndicho chanzo cha nyumba nyingi kuyumba au kusambaratika kabisa. Unajua sababu gani?

Nakuuliza acha kunitumbulia mijicho kama fundi saa aliyepoteza lensi. Siku zote sisi wenyewe ndiyo tumekuwa wanga wa uhusiano na ndoa zetu bila kujua.

Hebu kaa chini nikupashe ili usichelewe, pamoja na kumpikia chakula kitamu basi ongeza cha ziada uamshe furaha na kumfanya mwenzako achanganyikiwe na kuona mambo mapya ya kimahaba.
Si wote mmepitia unyagoni na kupata mafunzo ya chumbani, jamani mafunzo ya chumbani ukiyajua nina imani ndoa yako kila siku itakuwa mpya. Katika maisha ya ndoa hasa ya chumbani lazima mwakwetu ujue wanaume wanapenda nini. Na hii utaijua pale mwanaume wako wa kwanza utakaye kula naye raha umuulize kijanja vitu gani wanaume wanapenda siyo kukurupuka kama unatoka kujisaidia kichakani.

Siku zote mjenzi mzuri hujifunza tabia za udongo ili akijenga nyumba isianguke haraka au kuweka nyufa. Hata katika mapenzi ukiwa faragha na mwenzako hebu jenga tabia ya kudadisi.
”Mpenzi nikikushika wapi unajisikia raha?” lazima atakujibu vilevile nawe una haki ya kumueleza mpenzi wako kuwa:

“Mpenzi wangu usisumbuke sana kunipapasa mwili mzima, mi sehemu zangu ni hizi, ukinigusa tu ni kama umetwanga pilipili lazima nikohoe.”

Umeona siyo mtu anakushika sehemu zingine wala hazina msisimko unamuacha pengine naye maimuna hajui lolote alipokushika ndipo uwezo wake wa kujua sehemu za kumsisimua mwanamke. Kwa vile hajui basi utajikuta mpaka mchezo unaanza mwili wako upo baridiii. Haipendezi hebu basi tuambiane ukweli ili kuzifanya nyumba zetu wakati wote kuwa na furaha.

Kuna maeneo mengi ya mambo ya chumbani unatakiwa kuyajua mkiwa kwenye uwanja wa fundi seremala. Unapoona hutendewi haki mweleze mwenzako ili ajue siyo kukaa kimya unaumia moyoni kumbe ulitakiwa kusema. Wengi hulalamika hawajawahi kufurahi tendo la ndoa tangu waolewe hata wengine kudiriki kusema huwa hawafiki mwisho wa safari, mmh! Kioja.

Narudia kauli yangu siyo wote wanaoyajua mapenzi, hebu muulize mtu aliyekuzidi amewezaje kufurahia mapenzi muda wote. Akiisha kueleza basi lifanyie kazi ndani, haki ya nani utashangaa kumuona mtu mzima akilia kama mtoto mdogo si kwa kupigwa bali kutu ya mapenzi imeondolewa sasa hivi chuma kimekuwa lainiii raha kila kona.

Utashangaa unapata ambavyo hukuwaza kupewa, la muhimu ni kukubali kujifunza na kuyafanyia kazi hakika kila siku ndoa yako itakuwa mpya.

Yangu yanatosha, ni mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu.

GPL

No comments: