Rajib Roy, mwenye miaka 16, kutoka Kolkata, Bengal Magharibi atawasili Manchester wikiendi hii kufanya majaribio Old Trafford baada ya kunga`muliwa na timu ya kusaka vipaji ya Man United.
Rajib alipigwa picha akiwa katika chumba anachoishi na mama yake na kaka yake huko Kolkata ambako amelelewa na mama yake kahaba pamoja na kaka yake, huku akionsha baadhi ya vitu wanavyomiliki.
Msaada kwake: Rajib na mama yake Rekha ambaye ni kahaba amemsaidia katika mafanikio yake ya soka baada ya kumpeleka shule
Rajib ambaye hamfahamu baba yake akiwa amesimama kwenye mlango wa chumba chao katika kitongoji Sonagachi , Kolkata, zamani kilijulikana kwa jina la Calcutta, Bengal Magharibi.
Kijana huyu mdogo alijifunza mpira katika mitaani magharibi mwa Bengal , lakini sasa anaelekea Old Trafford
KIJANA mmoja nchini India aliyekulia mazingira duni, huku mama yeke mzazi akiwa anajiuza mwili wake (kahaba), Rajib Roy amechaguliwa kwenda kufanya majaribo ya soka katika klabu ya Manchester United ya nchini England.
Rajib Roy, anayelala chumba kimoja na mama yake na kaka yake katika wilaya moja ya Kolkata Bengal Magharibi amebahatika kupata nafasi hiyo adimu ya kwenda Old Trafford baada ya timu ya kung`amua vipaji kugundua uwezo wake.
Roy mwenye miaka 16 ni miongoni wa wachezaji 11 wanaotarajia kuwasili nchini England wikiendi hii na watatumia wiki mbili kufanya majaribio chini ya makocha wa Manchester United.
Kijana huyo mwenye kipaji kikubwa alinaswa na timu ya kusaka vipaji ya Manchester United katika mashindano ya kitaifa ya kusaka mchezaji bora wa India kwa vijana wadogo.
Vijana wengi wanaosafiri kwenda Manchester wikiendi hii wametoka familia bora zenye uwezo wa kuwasomesha na wanajua kiengereza vizuri.
Rajib kwa upande wake amekulia katika mazingira duni na kwa muda mrefu amekuwa akicheza mpira peku katika mitaa ya Kolkata.
Anaishi
Kijana huyo anaishi kitongoji cha Sonagachi ambacho kina makahaba wapatao elfu kumi na mbili(12,000) na analala kwenye chumba kidogo na mama yake Rekha na kaka yake.
Rajib anafananishwa na nyota wa Chelsea, Mbrazil Oscar ambaye alitoka mazingira duni mno huko kwao.
Kama ilivyo kwa watoto wengi wa mtaani, Rajib hamfahamu baba yake, na baada ya kusikia Manchester United imemchagua amehisi kuwa ndio baba yake.
Marafiki zake wengi wameishia katika matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu mwingine, lakini Rajib anashukuru sana kipaji chake cha soka kwani kinamfanya akose muda wa kufanya uovu huo.
Maisha yake yalibadilika miaka miwili iliyopita baada ya mama yake kumpeleka katika shule maalum kwa watoto wa makahaba iitwayo Rahul Vidya Niketan .
Shule hii ilianzishwa na kamati ta Durbar Mahila Samanwaya (DMSC) nchini India kwa lengo la kuboresha maisha ya watoto wa makahaba.
Miaka minne iliyopita mwanzilishi wa DMSC , Dr Samarjit Jana alianzisha mpango maalum wa soka ambao ungewaunganisha watoto wa makabaha na watoto wenye maisha mazuri katika jamii.
Mapema mwaka huu, mshambuliaji Rajib alikuwa miongoni mwa wachezaji wa Timu ya Magharibi mwa Bengal walioshinda kombe la Taifa la Watoto wanaoishi mazingira maguni kwa mchezo wa soka lililofanyika mji wa Nagpur.
Mwezi uliopita, Rajib na wenzake 30 walichaguliwa na DMSC kwenda kushiriki michuano ya Taifa ya shule za India katika mji wa Goa.
Makocha wa Manchester United walikuwa wanatazama michuano hii na kuchagua vijana 11 ambao watasafiri jumapili kwenda Old Trafford kufanya majaribio akiwemo na Rajib.
Rajib baada ya kuchaguliwa amesema kuwa:”watu wanazidi kuniuliza kuwa nimejisikiaje kuwa mtoto wa mama na kupata nafasi kama hii. Sijui jinsi ya kujibu swali hili. Lakini kocha wangu aliponiambia nimechaguliwa na Manchester United, ilikuwa kama nimepata baba vile”.
Aliongeza: “Mama yangu ni mtu wa aibu sana. Mara nyingi alinifungia ndani ili nisiharibikiwe na maisha, lakini nilijitahidi kutoroka na kwenda kucheza na wenzangu”
“Mwezi uliopita nilikuwa miongoni mwa vijana 30 waliochaguliwa kwenda kuweka kambi Goa kwa ajili ya mashindano ya shule ya kitaifa. Nilifika kwa kuchelewa kwasababu nilipanda treni kutoka Kolkata. Kila mtu alisafiri kwa ndege”.
1 comment:
hamna habari njema zaidi za kuzalilisha watu hata kama ni ukweli kwamba mama yake anafanya kazi hiyo mbaya lakini hakuna story nzuri zaidi ya hiyo kuweni kiakili
Post a Comment