Nakala ya barua ya kutisishwa kwa mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika Zanzibar kesho ukiongozwa na viongozi wa UKAWA ambayo unaweza kuiona kwa kubofya hapa, inasomeka ifuatavyo:-
YAH: TAARIFA YA KUSITISHWA MKUTANO WA HADHARA
Naomba urejee barua yangu Kumbu. Nam. W/MGH/SO/7/2/A/4 ya tarehe 17 Aprili, 2014 inahusika.
Ninakujulisha rasmi kuwa mkutano huo uliokuwa ufanyika kesho tarehe 19 Aprili, 2014 hapo Viwanja ya Demokrasia Kibanda Maiti umesitishwa kwa sababu za
KIUSALAMA WA NCHI.
Kwa barua hii unatakiwa kuwajulisha Wanachama na wapenzi wote wa Chama kuwa watulivu kwa muda huu, hadi hapo hali itakapo ruhusu kufanyika tena kwa Mkutano huo.
Tafadhali nawasilisha.
RAMADHANI S. NGAMIA - SSP
MKUU WA POLISI,
WILAYA YA MAGHARIBI UNGUJA.
------------ Mwisho wa kunukuu taarifa ya sitisho hilo. ------------
Katika taarifa ya habari iliyosomwa saa 2 usiku wa leo kupitia TBC, imeelezwa kuwa Jeshi la Polisi Zanzibar limesitisha mikutano yote ya hadhara ya vyama vya siasa visiwani humo.
Taarifa hiyo imetolewa na Kamishna wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame, wakati alipokutana na viongozi waandamizi wa vyama vya CCM na CUF katika makao makuu ya Jeshi la Polisi, Ziwani, Zanzibar.
Kabla ya kutolewa tamko hilo CUF ilipanga kufanya mkutano kama ilivyoelezwa hapo juu, wakati UV-CCM ilipanga kufanya mkutano wa hadhara keshokutwa, Jumapili katika eneo la Mabata.
No comments:
Post a Comment