Advertisements

Monday, April 21, 2014

TANESCO NJOMBE WANASA WEZI WA NYAYA ZA UMEME KITUO CHA MKOA HUO

Na Gabriel Kilamlya Njombe

Shirika la Umeme Tanesco Wilaya ya Njombe Leo Limefanikiwa Kuwanasa Watu Wawili Waliokutwa Wakiiba Nyaya za Umeme Katika Kituo cha Kusambazia Umeme Yaani Power Station Mjini Njombe Huku Wawili Wakihusika Katika Tuhuma Tofauti Ikiwemo Ya Kununua Nyaya Hizo na Mmoja Kushindwa Kuwajibika Kama Mlinzi wa Zamu.
Tukio Hilo Limetokea Majira ya Saa Nne Asubuhi Huko Katika Mtaa wa Uzunguni Kwenye Kituo Hicho cha Umeme Yaani Power Station Ambapo Vijana Wawili Wamekatwa na Mmoja Ametokomea Kusiko Julikana Wakati Wa Msako Huo.

Akizungumza Mara Baada ya Kuwafikisha Kwenye Kituo cha Polisi Mjini Njombe Msimamizi wa Shirika la Umeme Wilaya ya Njombe Bwana Renatus Henerico Amesema Kuwa Wizi wa Nyaya Hizo Ulianza Tangu Wiki Iliyopita Lakini Kutokana na Kuweka Mtego wa Kuwanasa Wezi Hao Leo Zoezi Hilo Limefanikiwa.

Bwana Renatus Amewataja Watuhumiwa Hao Kuwa ni Pamoja na Justin Kyando Mwenye Umri wa Miaka 17 Mkazi Wa Ramadhani Mjini Njombe,Gehazi Kilumbe Mwenye Umri wa Miaka 18 Ambaye naye ni Mkazi wa Mtaa Huo wa Ramadhani,Felista Ngota Ambaye ni Mnunuzi wa Nyaya Hizo Pamoja na Anna Mhenga Ambaye Alikuwa Mlinzi wa Zamu Katika Lindo Hilo.

Aidha Amemtaja Castory Mligo Kuwa Ametoroka wakati Wa 
Tukio Hilo na Kwamba Miongoni Mwa Vijana Hao Wawili Walikuwa Wafanyakazi wa Mkataba Mfupi Katika Shirika Hilo Yaani S.T.E Ambapo Baada ya Mkataba Wao Kuisha Wakaanza Kujihusisha na Matukio Hayo.

Pamoja na Mambo Mengine Amesema Kuwa Nyaya Hizo Zilizo Ibiwa Hadi SasaZinagharimu Zaidi Ya Shilingi Milioni 60 Kwani Walianza Kuiba Tangu Siku Nyingi.

Blog hii Imefanikiwa Kuzungumza na Mmoja wa Watuhumiwa Hao Anayefahamika Kwa Jina la Justin Kyando Ambaye Amesema Kuwa Wamekuwa Wakiiba Nyaya Hizo naKuziuza Kwa Mfanyabiashara Huyo Felista Ngota Ambaye ni Mnunuzi wa Vyuma ChakavuKatika Mtaa wa Msichoke Mkabala na Chuo Kikuu cha Amani Mjini Njombe.

Bwana Christian Mlelwa ni Mkuu wa Ulinzi Katika Kampuni Ya Jirani Security GroupYenye Makao Makuu Yake Jijini Dar es Salaam Ambaye Amesema Amekuwa Akimuomba 

Mkurugenzi wa Kampuni Hiyo Kumuongezea Walinzi Hususani Katika Eneo Hilo la PowerStation Lakini Hakuna Utekelezaji Wowote Kwani Eneo Hilo ni Kubwa Zaidi.

No comments: