Advertisements

Wednesday, April 16, 2014

Trafiki Ikulu waongoza waandishi


 
Kwa ufupi
  • Yawasindikiza wanahabari hadi ofisini kwao kwa msafara wa pikipiki za polisi

Dar es Salaam. Katika hali isiyo ya kawaida juzi jioni, Ikulu iliwasindikiza waandishi wa habari kurejea ofisini kwao kwa kutumia askari wa usalama barabarani, waliowaongoza ili kukwepa msongamano wa magari.
Hatua hiyo ilitekelezwa muda mfupi baada ya
katibu mkuu kiongozi (KMK), Balozi Ombeni Sefue kukutana na waandishi na kuwaonyesha Hati ya Muungano iliyozua mvutano kati ya wajumbe wa Bunge Maalumu.
Waandishi hao wa habari wa gazeti la Mwananchi na Citizen, Star Tv, Televisheni ya Taifa (TBC1) na Sibuka Tv, wakiwa kwenye magari ya kampuni zao, waliongozwa na pikipiki za kikosi cha usalama kama inavyokuwa kwa misafara ya viongozi wa kitaifa.
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Salva Rweyemamu alisema lengo la kutumia askari hao lilikuwa kuhakikisha wanawahi kuandika habari iliyohusu hati hiyo. Tukio hilo halikuwahi kufanywa na Ikulu.
Mkutano kati ya Sefue na wanahabari ilikuwa uanze saa 10:00 jioni, lakini ulichelewa na kuanza saa 11:05 jioni ukamalizika saa 11:35.
Ndipo Rweyemamu akawasiliana na askari husika, kuagiza pikipiki moja iliyotumika kuongoza wanahabari ili kukwepa foleni ambayo mara nyingi majira hayo huwa kubwa zaidi. Msafara ulipita kwenye Barabara za Mwai Kibaki, Ali Hassan Mwinyi, Sam Nujoma na kuishia barabara ya Mandela eneo la Mabibo External.
Pamoja na kuwapo msongamano wa magari barabarani, kwa msaada wa pikipiki hiyo safari ya kutoka Ikulu hadi Tabata Relini zilipo ofisi za Kampuni ya Mwananchi Communication Ltd, ilitumia dakika 28 tu; kuanzia saa 12:48 jioni hadi saa 1:15 Jioni.
Magari ya kampuni za TBC, Star Tv na Sibuka Tv yalikuwa yakichepuka na kuachana na msafara huo kila yalipokuwa yakikaribia kufika katika ofisi zao, huku wanahabari wa Mwananchi wakiongozwa hadi eneo la Mabibo External.

1 comment:

Anonymous said...

Wajamani haya mambo ni kuendeleza tu yaliyopita atuna jipya. Wakiandamana waafunzi mabomu, vyama vya siasa, mabomu! Sasa haki umekalia upande gani zaidi kwani hili swala ni kungangania serikali mbili tu basi wapeni wananchi uhuru wa katiba yao kwani viongozi mnachopigania hapo ni nini tunataka tukielewe msiwaburuze waTanzania. Asante. Kwani hiyo hati mnataka idumu milele? Tuendeni na wakati.