Advertisements

Friday, April 25, 2014

VIJANA 72 WA VIPAJI VYA SOKA KUTOKA NCHI 12 ZA BARANI AFRIKA WAANZA KUNOLEWA CHAMAZI DAR

Kocha Andrew Stokes kutoka shule ya soka la vijana ya Manchester United, akitoa maelekezo kwa washiriki wa kliniki ya Kimataifa ya soka ya Airtel Rising Stars inayofanyika kwenye uwanja wa Azam Compex jijini Dar es Salaam.
Washiriki mbalimbali wa Kliniki ya soka ya Kimataifa ya Airtel Rising Stars wakiwa kwenye mafunzo ya kliniki hiyo kwenye Uwanja wa Azam Complex.
Wakiendelea kupata maelekezo..
Kocha Andrew Stokes kutoka shule ya soka la vijana ya Manchester United, akitoa maelekezo kwa washiriki wa kliniki ya Kimataifa ya soka ya Airtel Rising Stars inayofanyika kwenye uwanja wa Azam Compex jijini Dar es Salaam.
Washiriki mbalimbali wa Kliniki ya soka ya Kimataifa ya Airtel Rising Stars wakiwa kwenye mafunzo ya kliniki hiyo kwenye Uwanja wa Azam Complex.
*Watakiwa kuiga mbinu za Manchester United
JUMLA ya Vijana 72 wenye vipaji vya soka kutoka nchi 12 Barani Afrika wanaoshiriki kliniki ya Airtel Rising Stars jijini Dar es Salaam wametakiwa kuiga mbinu zinazofundisha na kutimiwa na shule za soka za klabu ya Manchester United ya Uingereza ili waweze kuwa wachezaji wazuri hapo baadae.

Mafunzo hayo yalioanza Jumatano kwenye Uwanja wa Azam Complex chini ya kocha mkuu Neil Scott kutoka katika shule za Manchester United.

Akitoa mafunzo hayo, Scott alisema lengo la mafunzo hayo ni kumfanya mchezaji kuwa mkubwa kisoka, kutoka na kujiona ni mtu muhimu na wa kipekee. ‘Mtindo huu wa ufundishaji ninautoa, utamfanya mchezaji ajione ni mtu muhimu na wakipee na kumpa hamasa ya kuwa na shauku ya kujiendeleza zaidi na kufanya mchezaji kuwa na ari ya kujifunza kutokana na makosa, tabia na mwenendo akiwa ndani na nje ya uwanja.’ Alisema Scott.

Scott alisema ili mchezaji kuwa mkubwa kisoka hana budi kujiendeleza na ili kufikia mafanikio ni muhimu kuiga mbinu za uchezaji zinazofundisha na shule za soka za Manchester United.

Kocha huyo aliongeza kuwa wachezaji hao watafundisha vipegele vitano muhimu ambavyo ni uwezo wa kiufundi, kufanya maamuzi ya haraka uwanjani, kujenga mwili na saikolojia.

Siku ya pili ya mafunzo hayo, yalikuwa ni ya vitendo ambapo wachezaji walifundishwa masuala ya ufundi na jinsi ya kumkabili mpinzani wakati wa mchezo na baadae walihudhuria mafunzo darasani yaliyolenga jinsi ya mchezaji kuwa mkubwa katika soka.

Aidha, kutokana na somo hilo la mchezaji kuwa mkubwa, lilitoa fursa kwa vijana hao kuzoeana na kwa pamoja wakapitia majina ya wachezaji wakubwa duniani na sehemu zao za uchezaji ndani ya uwanja.

Katika kliniki hiyo ambayo inafikia tamati Jumapili, Tanzania ambao ndio wenyeji wanawakilisha na washiriki 19. Kumi 16 ikiwa ni wasichana ambao walishinda tawi la michuano ya Airtel Rising Stars barani Afrika Agosti mwaka jana Lagos na wavulana watatu.
Credit:Credit:Sufiani Mafoto

No comments: