ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, April 27, 2014

YANGA SC YAIKANDAMIZA SIMBA 4-2 SHEREHE ZA MUUNGANO HOUSTON

Ikimtumia mshambuliaji wa kukodi kutokea Burundi , Erick Niyonzima jioni ya leo katika kuadhimisha miaka 50 ya Muungano timu ya mashabiki wa Yanga SC wa Houston wamewabanjua wenzao wa Simba SC kwa mabao 4-2. Hadi mapumziko Yanga ilikuwa inaongoza kwa mabao 3-0 ambayo mawili yalifungwa na Erick na moja likifungwa na Ally Mtumwa.Kipindi cha pili Simba walikuja juu kutaka kusawazisha mabao yao na kupata mabao mawili yaliyofunga na Rahim Chomba na Ben Rulegura.Yanga walipata bao la nne dakika ya 88 ya mchezo likifungwa na erick tena baada ya kumfungisha tela beki mstaarabu Twahiru Muddy.Hadi kipenga cha mwisho cha Muamuzi Shaali kutoka Wichita kinapulizwa Yanga SC waliondoka kidedea.Timu zote leo zilitumia jezi mpya zilizotolewa na kampuni ya Delina Group ya Dar es Salaam chini ya mwenyekiti wake ndugu Davies Mosha.Pata taswira:

Kikosi cha Simba SC 
Kikosi cha Yanga SC
Wachezaji wa Simba na Yanga kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa THC Bi.Nuru Mazora

Bi.Tunu na Bi.Nuru Mazora walikuwepo kushangilia mechi

1 comment:

Anonymous said...

mshakuwa watu wazima nyinyi wadada kwanini mnajihashua au kuna mnachokipata kwa huu muungano