Advertisements

Friday, May 2, 2014

19 wauwa katika mlipuko Nigeria


Waliojeruhiwa walikimbizwa hosipitalini
Maafisa nchini Nigeria wanasema kuwa watu 19 wameuawa baada ya mlipuko kutokea katika kituo cha basi katika mji mkuu wa taifa hilo Abuja.
Kwa mujibu wa mkurugenzi wa idara ya kushughulikia mikasa na hali ya dharura- FEMA- Abbas G Idriss, watu 60 walijeruhiwa vibaya lakini sitaka kati yao wametibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani. Amesema kuwa magari sita yameharibiwa katika mlipuko huo.
Mlipuko huo umetokea katika eneo la Nyanya, karibu na kituo cha
basi ambako zaidi ya watu sabini waliuwawa katika shambulizi la tarehe14 mwezi Aprili.
Ripoti za awali zimesema kuwa watu kadhaa wameuwawa na wengine wengi kujeruhiwa.
Waandishi wanasema kuwa mlipuko huo umesababishwa na bomu lililotegwa ndani ya gari. Mmoja wa walioshuhudia kisa hicho amesema aliona miili 20 ya watu waliouwawa. Hakuna kundi lililodai kuhusika katika shambulizi hilo lakini kundi la wanamgambo wa kiislamu la Boko Haram limewahi kutekeleza mashambulizi kama hayo mjini Abuja
Mengi ya mashambulizi ya Boko Haram yamekuwa yakitokea katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa Nigeria.
Lakini shambulizi la bomu la tarehe 14 Aprili lilizua hofu kwamba huenda wanamgambo hao wameanza kupanua maeneo wanayoendeleza harakati zao.

No comments: