ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, May 8, 2014

BALOZI MDOGO MHE. OMAR MJENGA AKUTANA NA MHESHIMIWA GELINA,BALOZI MDOGO WA MALAWI, DUBAI NA UJUMBE WAKE

 Mheshimiwa Omar Mjenga na wageni wake, wakiwa katika mazungumzo, ambayo yalilenga kubadilishana mawazo kuhusu uendeshaji wa Balozi Ndogo. Aidha, walizungumzia njia muafaka za kuvutia watalii na uwekezaji katika nchi zao.
 Ujumbe huu, awali, ulishakutana na Balozi Mdogo wa Afrika Kusini, Angola, Mozambique, Ethiopia, China, India, na Marekani.Wanaendelea na mikutano yao wikiijayo.
Mheshimiwa Oamr Mjenga  akiwa katika picha ya pamoja na wageni wake. Kulia kwake ni Mheshimiwa Bi Gelina Balozi Mdogo wa Malawi. Nakulia kwa Mheshimiwa Gelina ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu (DAP) kutoka wizara ya mambo ya nje ya Malawi. Kushoto kabisa mwa picha ni Mhasibu Mkuu wa wizara hiyo na kulia mwa picha Naibu Mkuu wa Itfaki kutoka wizara ya mambo ya nje ya Malawi.

No comments: