Bibi wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole akipelekwa mahakamani.
BIBI wa Kinigeria, Olabisi Ibidun Cole (65), leo ameangua kilio katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar ers Salaam wakati akipelekwa kizimbani kwa ajili ya kusomewa kesi yake ya kunaswa na madawa ya kulevya yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 37.
Hakimu aliyepelekewa kesi hiyo, Frank Mushi, aliiahirisha kesi hiyo mpaka kesho ili bibi huyo ambaye hajui Kiswahili wala Kiingereza atafute mkalimani.
Cole alisema lugha anayoweza kuitumia kiufasaha ni Kiyoruba ambacho hutumiwa nchini Nigeria. Katika hali iliyoonesha kukata tamaa, bibi huyo alianza kuangua kilio akiomba Mungu amsaidie.
(PICHA NA RICHARD BUKOS/GPL)


2 comments:
Hivi mtu mwenye miaka 65 ni bibi? Kama hivyo ndivyo basi taifa linaongozwa na mabibi na mababu kwani zaidi ya asilimia 80 ya viongozi wetu ni over 60
Huyu mama asiejua hata kiswahili alikuja kufanya nini, na lazima alikuwa na mtu/watu walio mu-host hapa nchini.Jeshi la polisi linatakiwa kuaanza kudeal na king pings wa hii biaashara.I f you want to get ride of a tree in your back yard you don't shred -off the leaves but rather you up root the whole thing.
Post a Comment