KAMATI MAALUM YA UCHAGUZI- DMV
2014
TANGAZO RASMI:
MABADILIKO YA TAREHE YA MWISHO YA
KURUDISHA FOMU ZA KUGOMBEA UONGOZI.
Kamati ya Uchaguzi wa viongozi wa Jumuia ya Watanzania-
Washington Metro (ATC), inawatangazia kuwa imeongeza muda wa wagombea uongozi
wa Jumuiya kurudisha fomu za maombi na viambatanishi vyote hadi Juni 6, 2014.
Hii pia itawapa muda wanajumuiya kujiunga na jumuiya yetu ili tuwe na uchaguzi
wa Kidemokrasia utakao fuata katiba tuliyojiwekea ili ituongoze. Tarehe ya
Uchaguzi bado ni Juni 21, 2014.
XXXXXXX KARIBUNI NYOTE XXXXXXXX
No comments:
Post a Comment