Akimtunuku nishani hiyo Rear Admiral Mathew Kohler ambaye ni Naibu Kamanda wa Kamandi ya Africa ya jeshi la marekani ( AFRICOM), alieleza kuwa nishani hii hutolewa na rais wa marekani kwa idhini ya Bunge ( Congress) kwa maafisa ambao utumishi wao umesaidia kuunganisha nchi zao na Marekani katika nyanja mbalimbali.
Nishani hiyo pia imeambatana na cheti na barua za idhini kutoka waziri wa ulinzi wa Marekani, waziri wa jeshi na Mkuu wa Mjeshi ya Marekani.
Akitoa shukrani zake, jenerali Maganga ambaye aliambatana na mke wake Love, alieleza furaha yake na kubainisha kuwa kimsingi alikuwa anatenda kazi alizoagizwa na kuwa ametunukiwa nishani hii ni jambo la kushukuru. Alieleza kuwa sifa hii pia iwaendee waheshimiwa mabalozi; Ombeni Sefue, Mwanaid Maajar na Liberata Mulamula ambao amefanya kazi chini yao kwa nyakati tofauti. Amewashukuru pia maafisa wenzake kituoni na wale wa Makao Makuu ya Jeshi na watumishi wa Umma ofisi ya Mwambata Jeshi

Pokea cheti hiki kuwa uthibitisho wa nishani niliyokukabidhi Nishani niliyokutunuku ni ya heshima kwako kwa kazi nzuri ya uwakilishi wa majeshi yako

Mrs Maganga akionesha cheti alichotunukiwa mum wake.

Baadhi ya maafisa wakuu walioshiriki hafla hiyo wakiongozwa na Brig. Gen Mabeyo

Kutoka Kushoto ni Admiral Kohler, Love Maganga, Brigedia Jenerali Maganga na Colonel Kevin Balisky Mwambata Jeshi wa marekani nchini.
Admiral Kohler akieleza sifa anazotakiwa kuwa nazo mtunukiwa
Baadhi ya maafisa wa jeshi la Marekani wakimsikiliza Brigedia jenerali Maganga
Cheti kiambatishi na nishani aliyotunikwa Brigedia Jenerali Maganga na Serikali ya Marekani

No comments:
Post a Comment